MASOMO YA MISA, FEBRUARI 9, 2023
ALHAMISI, JUMA LA 5 LA MWAKA
SOMO 1
Mwa. 2:18 – 25
Bwana Mungu alisema, Si vema huyo mtu awe peke
yake, nitamfanya msaidizi wa kufanana naye. Bwana Mungu akafanyiza kutoka
katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu
ilia one atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina
lake. Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufungwa, na ndege wa angani, na
kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsmaidia Adamu aliyefanana
naye. Bwana Mungu akamletea Adamu aliyefanana naye. Bwana Mungu akamletea Adamu
usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama
mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya
mwanamke, akamleta kwa Adamu.
Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa
yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana metwaliwa
katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye
ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Nao walikuwa uchi wote wawili,
Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 128:1 – 5 (K) 1
(K) Heri kila mtu amchaye Bwana.
Heri kila mtu amchaye Bwana,
Aendaye katika njia yake.
Taabu ya mikono yako hakika utaila,
Utakuwa heri, na kwako kwema. (K)
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,
Vyumbani mwa nyumba yako;
Wanao kama miche ya mizeituni
Wakiizunguka meza yako. (K)
Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.
Bwana akubariki toka Sayuni,
Uone uheri wa Yerusalemu
Siku zote za maisha yako. (K)
SHANGILIO
Zab. 119:135
Aleluya, aleluya,
Umwangazie mtumishi wako uso wako, na
kunifundisha amri zako.
Aleluya.
INJILI
Mk. 7:24 – 30
Yesu aliondoka Nazareti akaenda zake hata mipaka
ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini
hakuweza kusitirika. Ili mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu,
alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake. Na yule mwanamke ni
Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katika binti yake.
Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha
watoto, na kuwatupia mbwa. Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata
mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto. Akamwambia, Kwa sababu ya neno
hilo, enenda zako; pepo amemtoka binti yako. Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta
yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA
MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright ©
1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of
Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha
ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment