“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Februari 9, 2023
Juma la 5 la Mwaka wa Kanisa
Mwa 2: 18-25;
Zab 128: 1-5;
Mk 7: 24-30.
KUDHIHIRISHA IMANI!
Kwanini Yesu anaongea na Mwanamke yule kwa jinsi ile? Mwanamke anakuja
kwake, pengine katika hali ya hofu, na kuanguka katika miguu yake, nakuomba
amponye mtoto wake. Anamwambia “si haki kuchukua chakula cha watoto na kutupia
Mbwa?” Kwanini alisema hivi?
Kwanza kabisa, tunapaswa kufahamu kila anachosema Yesu ni kitendo cha
upendo. Ni kitendo cha huruma kuu na ukarimu. Tunafahamu hivi kwasababu ndivyo
Yesu alivyo. Yeye ni upendo wenyewe. Sasa twawezaje kupatanisha mchanganyo huu?
Ufunguo wa kufahamu mchanganyo huu ni kutazama matokeo yake. Tunapaswa
kuangalia jinsi huyu Mwanamke alivyo mjibu Yesu na jinsi mazungumzo yalivyo
isha. Tukifanya haya, tunaona kwamba mwanamke huyu amejibu kwa imani na
unyenyekevu mkubwa. Anachosema Yesu ni ukweli, tunaweza kusema kwamba
alichosema ni kwamba hakuna mwenye haki ya huruma yake na neema. Hakuna, kwa
mama yule pamoja na mtoto wake, ya kwamba “wanastahili” Mungu kufanya kazi
katika maisha yao. Yesu anatambua hili, na kwa kusema alichosema, alimpa mama
huyu nafasi ya kuonyesha imani yake kubwa ili wote waweze kuona. Kwa maneno
yake yalimfanya angae kwa imani yake, matumaini na kuamini. Hili ndilo lilokuwa
lengo la Yesu na kweli lilifanikiwa. Lilifanikiwa kwasababu alivyokuja kwa
Yesu, Yesu alitambua kwa hakika alikuwa na imani kubwa. Alifahamu atajibu kwa
unyenyekevu na kwa imani. Mwanamke huyu alifanikiwa na sisi pia tunaweza
kushuhudia juu ya imani yake kubwa na unyenyekevu.
Tujitahidi kujiweka kwa viatu vya mwanamke huyu na tumsikie Yesu akiongea
maneno haya haya kwetu. Je, utajibu nini? Tutajibu kwa hasira na chuki? Je,
majivuno yetu yataumizwa? Au tutajibu kwa unyenyekevu wa ndani, na kutambua
kuwa kila tunachopokea kwa Mungu ni zawadi na kwamba sio haki yetu? Kujibu
namna hii ni kitendo cha imani ambayo Mungu anaisubiri kutoka kwa kila mmoja
wetu na ni ufunguo wa kupokea huruma yake tunayo hitaji.
Sala: Bwana, naomba uninyenyekeshe. Tupa mbali majivuno yangu. Nisaidie
niweze kuanguka miguuni mwako. Nisaidie niweze kukusadiki kwamba umependezwa na
mapendo yangu kwako, ufungue wingi wa neema zako na kumimina juu yangu. Yesu,
nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment