MASOMO YA MISA, FEBRUARI 17, 2023
IJUMAA, JUMA LA 6 LA MWAKA WA KANISA
SOMO 1
Mwa. 11:1 – 9
Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi
ya Shinari; ;wakakaa huko. Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome
moto. Walikuwa na matofali badala yam awe, na lami badala ya chokaa. Wakasema,
Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilelel chake kifike mbinguni, tujifanyie
jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akashuka ili auone mji
na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni
taifa moja, na lugha yao ni moja; na hayo ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa
hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie
usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. Basi Bwana akawatawanya kutoka
huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina
lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote;
na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 33:10 – 15 (K) 12
(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa,
Huyatangua makusudi ya watu.
Shauri la Bwana lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi. (K)
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia. (K)
Toka mahali pake aketipo,
Huwaangalia wote wakaao duniani.
Yeye aiumbaye mioyo yao wote
Huzifikiri kazi zao zote. (K)
SHANGILIO
Zab. 119:13
Aleluya, aleluya,
Umwangazie mtumishi wako uso wako, na
kunifundihsa amri zako.
Aleluya.
INJILI
Mk. 8:34 – 9:1
Yesu aliwaita mkutano pamoja na wanafunzi wake,
akawaambia, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike na
msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza,
na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu
ataisalimisha. Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata
hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe ini badala ya nafsi yake? Maana kil amtu
atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na
dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa
Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika
hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa
Mungu umekuja kwa nguvu.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA
MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright ©
1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of
Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha
ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment