"ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Februari 17, 2023
Juma la 6 la Mwaka wa Kanisa
Mwa 11: 1-9;
Zab 33: 10-15;
Mk 8:34 – 9:1.
KUMFUATA YESU!
Katika Injili ya leo Yesu anatuambia sisi wafuasi wake tubebe misalaba yetu
tumfuate. Kumwamini Yesu, si kukubali mafundisho yake tu kuwa ni ya kweli na ya
kuaminika, bali kuyatenda. Katika hali ya kawaida, kila mtu aliyesoma Injili ya
leo atakuwa amejibu swali hili katika hali tofauti ya maisha yake. Kila wakati
uendapo kanisani, unapo tumia muda kusali, au kusoma Maandiko Matakatifu kwa
njia moja au nyingine, hata mara nyingi tumesali sala mbali mbali tukiweka
akili zetu kuamua kumchagua na kumfuata Kristo. Lakini tunapaswa kufanya zaidi
ya kufanya uchaguzi wa kiakili tu katika ujumbe wa Injili hii.
Neno, “Kila apendaye” linaonekana kufunua zaidi ya kuamua tu, linaonesha
pia kutamani. Linaonesha kuwa ile tamaa ya kumfuata Yesu sio kila wakati ni
hatua ya kwanza katika kumwelekea, ni ya mwisho. Hatua ya kwanza inapaswa kuja
katika hali ya kuelewa ukweli na kuukiri. Pili, tunapaswa kufanya kile tulicho
chagua. Tatu, wakati neema imeanza kufanya kazi ndani yetu tunaanza “kutamani”
yote anayotaka Yesu kwetu na yote aliotuitia tuyafanye. Kwa hiyo ni uamuzi
ghani tunao jikuta sisi wenyewe tukifuata tunapo amua kumfuata Yesu kwa moyo
wetu wote? Tutajikuta tukitamani kile alichofunua Yesu, kujikana wenyewe,
kuchukua misalaba yetu na kufuata nyayo za Yesu. Je, unatamani hicho?
Ni rahisi kutamani kupenda na kupendwa, katika hali ya kawaida kabisa. Ni
matumini kwamba, sisi wote tunapenda kufurahia maneno ya ukarimu na maneno ya
kujali, tukiyatoa na kuyapokea. Lakini kwa upendo wa Yesu unahitaji kufuata
mfano wake wa upendo, unapenda wewe upende zaidi kuliko hata kujipenda
mwenyewe, upendo wa sadaka. Huu ndio ukamilifu wa upendo! Tunaitwa, kupenda bila
kuangalia gharama, bila kujali malipo tunayopata. Au pia katika hali ya juu
kabisa tunaitwa kupenda hata kile kinacho tusababishia maumivu na ugumu
inapofika ni kutimiza mapenzi ya Mungu. Mapenzi yake yanahitaji matendo ya
sadaka. Upendo wa kweli unafanya hata zaidi ya haya.
Je, unapenda kumfuata Yesu na upo tayari kukumbatia yote anayotaka
tuyafanye. Sema “ndio” kwake na msalaba wake. Mwishoni utapata uzima na furaha
ya milele.
Sala: Bwana, ninatamani msalaba wako. Ninataka kufikia kiwango cha upendo
ambao utanifanya nijikabidhi kwako kabisa, bila kuhesabu gharama, na kutamani
matendo yanayo hitaji sadaka kubwa. Ulibeba msalaba wako bila kujibakiza
kwasababu ya upendo wako kwetu. Nisadie niweze kuiga mfano wako kamili. Yesu
nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment