“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Februari 3, 2023
Juma la 4 la Mwaka wa Kanisa
Ebr 13: 1-8;
Zab 27: 1, 3, 5, 8-9;
Mk 6: 14-29.
CHAGUA KULINDA MAISHA!
Leo tunaona mwisho na unyong'onyevu wa mwenye haki na asiyeogopa nabii wa
kweli Yohani Mbatizaji katika mikono ya mtawala dhalimu, aliye jazwa na tamaa,
na picha ya utukufu dhalimu wa uongo wa hadhi na heshima! Herode alifanya
makosa makubwa matatu, ambayo mtawala mwenye kuwajibika hapaswi kufanya hivyo.
Kwanza, yeye alionesha mfano mbaya, kwa kumuoa mke wa nduguye. Pili, yeye
alifanya ahadi ya bila kufikiri kwa yule msichana aliyecheza. Tatu, alihofu
watu watasema nini na kujaribu kuokoa heshima yake ya uongo, aliamuru mauaji ya
mtu mwenye haki asiye na hatiya. Yohane Mbatizaji.
Hakuna mtu mwenye haki ya kucheza na maisha ya mtu mwingine, iwe katika
gereza au katika mitaa au akiwa tumboni. Na waliopo katika madaraka, wana
wajibu wa kulinda maisha, na wanalazimika kufikiri mara mbili na kufanya hakika
kwamba maisha hayapo hatarini.
Tutafakari leo, kuhusu hali zetu za kila siku za maisha. Je, unapatwa na
hasira na kujifanya kuielekeza kwa wengine ambao hawastahili? Tutafakari juu ya
tabia hizi na tuangalie kwa undani chanzo chake. Kama ukiona chanzo cha tabia
hii ambayo sio nzuri pengine ni kwasababu ya dhambi yako mwenyewe ya maisha
yako, tubu kwa hakika na kuimaliza ili Bwana wetu akuweke huru kutoka katika
malipo yake.
Mara moja nyuki, ambaye mwenendo wake ulikuwa mzuri na kama asali
anayofanya, alikwenda kwa Mungu na kumuomba mafanikio akisema. "Naomba
ninapo muuma mtu afe hapo hapo." Mungu akashtuka. Mafanikio mara moja
yakabadilishwa na kuwa laana. "Mungu akasema ni sawa. Lakini yule atakayeuma
ndiye atakayekufa sio yule atakayeumwa” "Mungu anapenda maisha ya endelee,
sio yaharibiwe.
Sala: Bwana, natubu dhambi zangu zote. Ninasali ili niweze kuziona dhambi
zangu kwa uaminifu kabisa na kwa kweli. Ninapo ona dhambi zangu, nisaidie
niweze kuziungama niweze kuwa huru na sio aliye elemewa na mzigo wa dhambi.
Bwana, ninaomba niyalinde maisha ya aina zote. Ninaomba nijitahidi kuwa mjumbe
wa maisha. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment