“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Februari 14, 2023
Juma la 6 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Wat. Sirili (Mtawa) na Metodi (Askofu)
Mwa 6: 5-8; 7: 1-5, 10;
Zab 29: 1-4, 9-10;
Mk 8: 14-21.
CHACHU ULIMWENGUNI!
Kila anaye andaa mkate anatambua jinsi ya chachu kidogo (Amira) inavyo
fanya kazi ndani ya donge la unga. Ukiweka kidogo tu ina umusha unga wote. Na
yote hii inatokana tu na hii chachu kidogo tu. Kwahiyo ni nini hii chachu ya
Mafarisayo na Herode? Ni maneno mabaya, maovu tena yenye makosa wanayo eneza.
Kwa Mafarisayo, inaweza kuwa ni kushindwa kumwelewa Yesu alivyokuwa akifanya na
kusema. Waliweza hata kubadilisha maneno yake kidogo tu na kuelezea kwa wengine
katika maana tofauti. Hii ni mbaya sana na ilikuwa na madhara kwa kila mtu kwa
wakati ule na baadae. Kidogo kidogo mbegu hiyo ndogo ya wasi wasi ingekuwa na
kuenea kwa wengine.
Tunawaza kufikiria juu ya yote hayo, tukafahamu pia watu wanaofanya hivyo
kwa wakati wetu. Lakini tunaweza kukosea kama hatujaanza kujiangalia sisi
wenyewe kwanza. Je, ninafanya haya wakati mwingine? Je, nimejikuta nikipindisha
ukweli kwa kutengeneza maneno ambayo huleta maana tofauti na jinsi mtu
alivyosema? Je, ninawaongoza wengine kwa maneno ya uongo wakati naufahamu
ukweli? Tunapaswa tuangalie maneno yetu na kutambua uzito uliopo katika maneno
hayo. Maneno machache yaweza kuleta madhara makubwa kwa kipindi kikubwa. Ni
vizuri kuwa na hali ya kupenda ukweli kwani kujaribu kupindisha ukweli huleta
madhara makubwa daima.
Lakini pia sio hilo tu tunalopaswa kufanya. Tunapaswa kutambua pia neno
dogo la upendo tunalosema limejaa utajiri mwingi ambao huweza kuleta mema na
neema kwa muda wote. Pengine ni tabasamu tu dogo tunalo onesha au kitendo cha
ukarimu ambacho tunadhani kinajiondokea tu bila kutambulika. Hili tabasamu dogo
na ukarimu mdogo ni chachu ya Injili. Inaleta tofauti na kuleta chachu njema
pia. Tutafakari juu ya mambo madogo tunayofanya katika maisha yetu. Tutambue
kuwa labda iwe dhambi ndogo inaleta madhara makubwa , au kiwe kitendo kidogo
cha upendo kinaleta Baraka kubwa mwishoni.
Sala: Bwana, nisaidie niweze kuwa mwaminifu na nisaidie niweze kutamua ni
chachu ghani ninayo ileta katika maisha ya kila siku. Nisaidie niweze kujitenga
na mabaya na unijaze mema. Nisaidie niweze kuwa chachu njema katika yote ninayo
sema nakutenda kila siku. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment