“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Januari 13, 2023
Juma la 1 la Mwaka wa Kanisa
Ebr 4: 1-5, 11;
Zab 77: 3-4, 6-8;
Mk 2: 1-12
WAKATI MUNGU AKIWA KIMYA
Yesu anawavuta watu kwake. Kuna watu wengi wanakuja kwa Yesu kiasi kwamba
hakukuwa na nafasi kwa kila mmoja, hata katika mlango wakuingia ndani
alikokuwa. Tunaweza kuwa na hakika kwamba wote waliokuja kumsikiliza hata kama
hawakuweza kuingia ndani, walipata baraka kwa Imani yao. Inafunua hamu ya
kiroho ya kuwa karibu na Yesu, na kuwa naye, huleta mabadiliko. Inawezekana
anatokea kwetu katika ukimya au tunaweza tusifahamu tunamtafuta wapi. Lakini
usikate tamaa kama hali hii imekuwa katika maisha. Ukweli ni kwamba hamu yako
ya kuwa na Mungu yenyewe ni zawadi kubwa, na ina mengi ya kubadili maisha yako.
Kuna nyakati katika maisha unahisi Mungu kuwa mbali, na mkimya na hujui pa
kumpata. Wakati hili linatokea, tutambue kuwa huu ndio muda wa kuja karibu
zaidi na Mungu kuliko siku nyingine zozote. Ni wakati ambao Mungu anataka
kutunongoneza ili tuweze kuwa na umakini wetu tena. Muda huo weka umakini wako
kwa Bwana zaidi na weka nia yako zaidi ya kutaka kuwa naye na kukuwa. Ni hamu
hii ya kuwa karibu zaidi na Yesu inaweza kuleta matunda mema zaidi katika
maisha yako hata zaidi kuliko ungemsikia kwa sauti kubwa zaidi.
Katika Injili tunaona uponyaji wa yule mwenye kupooza unamfanya Yesu apate
upinzani. Yesu ambaye ni mwenye nguvu katika maneno na matendo, uwezo wake wa
kusamehe dhambi unathibitishwa na uwezo wake wa kuponya mtu aliyepooza. Yesu
ambaye ni Masihi, mtawala wa kweli na Mfalme wa Israeli, Mwana wa Mungu
amekataliwa.
Katika maisha yetu pia, sisi tunafurahi tukiwa katika utumwa wa dhambi,
nguvu, milki na anasa, badala ya kuwa katika uhuru wa kuachana na mambo hayo.
Tuko tayari kukataa furaha ya milele kwa ajili ya kitu cha muda mfupi na cha
haraka. Leo, Yesu anatuhimiza tumchague yeye kuliko yote tunayoyapenda. Je!
Tunayo Imani ya kukataa yote yanayotutenga na Mungu kwaajili ya Yesu?
Sala: Bwana, naomba unifanya mimi niwe na uwezo wa kukuchagua wewe kuliko
yote yanayopita ya Ulimwengu huu. Ongeza hamu yangu ya kutaka kuwa karibu nawe
zaidi. Nisaidie nikutamani wewe zaidi ya yote. Nisaidie niache yote ambayo
yananiweka mbali nawe na naomba nikupe umakini wangu wote. Yesu nakuamini wewe.
Amina
No comments:
Post a Comment