ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Januari 27, 2023
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa
Ebr 10: 32-39;
Zab 37: 3-6, 23-24, 39-40;
Mk 4: 26-34
MBEGU ZA UFALME WA MUNGU!
Leo Yesu anaelezea habari ya mtu anaye mwaga mbegu zake ardhini. Ikisha
oteshwa, anasubiri mpaka itakavyo ota na kukuwa na kutoa mavuno. Haelewe ni kwa
jinsi ghani zinavyokuwa, lakini siku ya mavuno ifikakapo anavuna. Yesu pia
anaongea kuhusu mbegu ya haradali. Hii ni ndogo sana lakini ina utajiri ndani
yake. Hii mbegu pamoja na kwamba ni ndogo sana ina utajiri ndani yake ya kuweza
kuwa mti mkubwa, na kuwa chanzo cha chakula kwa ajili ya ndege na sehemu ya
kupumzikia ya ndege.
Huu ni ni kukweli unao dhihirisha kwamba Yesu anapenda kumtumia kila mmoja
wetu katika kujenga ufalme wake. Tunaweza kujisikia kwamba hatuwezi kufanya
mengi sana, na kwamba hatuja pewa vipaji vingi kama wengine, na kwamba hatuwezi
kuleta mabadiliko makubwa, lakini hii sio kweli. Ukweli ni kwamba kila mmoja
wetu amepewa vipaji vingi vya ajabu na Mungu ambavyo Mungu anapenda vizae
matunda. Anataka alete kutoka ndani mwetu vitu vya utukufu kwa ajili ya
Ulimwengu. Tunachopaswa kufanya ni kumruhusu yeye afanye kazi ndani yetu. Kama
mbegu, tunapaswa tujiruhusu wenyewe kujiotesha kwenye udongo wa huruma yake kwa
njia ya Imani na kujikabidhi kwenye mapenzi yake. Tunapaswa tujimwagilie kwa
sala za kila siku na kuruhusu mwanga wa wake utuangazie ili aweze kuvuna
matunda apendavyo kutoka ndani yetu na alicho otesha tangu kuumbwa kwa
ulimwengu.
Ametufanya sisi kwa lengo la kuleta Ufalme wake ndani yetu. Ni jukumu letu
kumruhusu Mungu afanye yote ndani yetu ambayo amepanga katika maisha yetu.
Sala: Bwana, nakupenda na ninakushukuru kwa yote uliotenda katika maisha
yangu. Ninakushuru kwa namna ya pekee, kwa yote, ambayo najua utatenda katika
maisha yangu. Ninakuomba ili niweze kujikabidhi kwako, ili uweze kunitakasa
mimi kwa neema yako, naomba ulete katika maisha yangu matunda mema. Yesu
nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment