MASOMO YA MISA, JANUARI 14, 2023
JUMAMOSI, JUMA LA 1 LA MWAKA
KUMBUKUMBU YA MT. DEVASAHAYAM PILLAI
SOMO 1
Ebr. 4:12 – 16
Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina
ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya
nafsi na roho, na ivungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi
kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi
mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na
mambo yetu.
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika
mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hatuna
kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeyey
alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na
tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya
kutusaidia wakati wa mahitaji.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 19:7 – 9, 14 (K) Yn. 6:63
(K) Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako.
Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako,
Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.
Umempa haja ya moyo wake,
Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake. (K)
Maana umemsogezea Baraka za heri,
Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Alikuomba uhai, ukampa,
Mda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. (K)
Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako,
Heshima na adhama waweka juu yake.
Maana umemfanya kuwa Baraka za milele,
Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako. (K)
SHANGILIO
Lk. 4:18 – 19
Aleluya, aleluya,
Bwana amenituma kuwahubiri maskini habari njema,
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao.
Aleluya.
INJILI
Mk. 2:13-17
Yesu alitoka, akaenda kando ya bahari, mkutano
wote ukamwendea, akawafundisha. Hata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa
Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.
Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake,
watoza ushuru wengi wa wenye dahmbi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake;
kwamaana walikuwa wengi wakimfuata. Na waandishi na Mafarisayo walipomwona
anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake,
Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Yesu aliposikia
aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita
wenye haki, bali wenye dhambi.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora
- Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are
published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings
are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment