Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUMLETA YESU KWA “WASIOMTAMANIKA”!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Januari 14, 2023
Juma la 1 la Mwaka wa Kanisa

Ebr 4: 12-16;
Zab 18: 8-10, 15;
Mk 2: 13-17


KUMLETA YESU KWA “WASIOMTAMANIKA”!


Katika Injili tunaona Yesu amemwita Mathayo (Lawi), mtoza ushuru, ambaye alikuwa anachukuliwa kama mtu aliye mbali na Ufalme wa Mungu, na anaitwa kuwa mwanafunzi wa Yesu. Lawi anaelewa thamani ya wito kutoka kwa Bwana na anataka kusherehekea na marafiki zake. Yeye anapanga sikukuu na amewaita marafiki zake, ili nao wapate kuitwa kufurahia ushirika wa kuwa na Yesu na wasitengwe mbali na huruma na msamaha wake.

Tunafurahi sana kuwanyoshea wengine vidole. Yesu pia alipingwa pia kwa kuwa karibu na wadhambi. Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu isipokuwa Yesu, ni mdhambi. Yesu kwa uhuru kabisa muda mwingi alikuwa na wale ‘wasio tamanika’/wasio pendwa . hakuogopa kuonekana kuwa na hawa waliotengwa na jamii. Yesu pamoja na wafuasi wake waliwakaribisha watu hawa. Walikula na kunywa na watoza ushuru, makahaba, nk. Zaidi ya hayo waliwakaribisha hawa watu bila ya kuwahukumu au kuwaonyoshea kidole.

Je, upo tayari kujihusisha na wale wasio maarufu, wasio na kitu, walio umizwa, walio changanyikiwa, na wengineo? Je upo tayari kupoteza umaarufu wako kwasababu ya upendo na kujali kwa wale wasio na kitu? Upo tayari kufanya yote na kusaidia hata wale unaojua watakuharibia jina lako? Tunaitwa kushuhudia ujumbe huu wenye nguvu kutoka kwa Yesu. Tunaitwa kuwa na nguvu ya ujumbe huu wa Yesu unao watafuta daima walio potea na anaye muita kila mmoja wetu kufurahia urafiki naye. Kama Matayo na wafuasi wa Yesu tunaitwa kuwaita kwa Yesu wote waweze kupata ukaribu wa Yesu pamoja nasi.

Sala: Bwana, unawapenda watu wote kwa mapendo ya ndani na upendo kamili. Ulikuja kwa ajili ya wale ambao maisha yao yalikuwa yamevunjika na wadhambi. Nisaidie niweze kuwatafuta wote walio wahitaji na kuwapenda wote kwa upendo usio na kipimo na kwa upendo usio wa kuhukumu. Yesu nakuamini wewe. Amina

Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment