“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatatu, Januari 16, 2023
Juma la 2 la Mwaka wa Kanisa
Ebr 5: 1-10;
Zab 110: 1-4;
Mk 2: 18-22.
MAISHA YASIO UNGWA, MAISHA MAPYA
Yesu anasema kwamba, hakuna anaye weka divai mpya katika viriba vya zamani,
kwani vitapasuka. Kwa hiyo, divai Mpya inawekwa kwenye viriba vipya. Hili
linaeleza kwetu kwamba kama tunataka kupokea ujumbe wa Yesu upya na ujumbe wa
Injili unao badili maisha, tunapaswa kuwa watu wapya. Maisha yetu ya zamani ya
dhambi hayawezi kuchanganywa na zawadi ya neema. Kwahiyo, kama tunataka kupokea
ujumbe wa Yesu, ni lazima kuunda maisha mapya sasa.
Yesu anawaonya wafuasi wake kuhusu “akili zilizo fungwa”, zinazo kataa kujifunza
kitu kipya. Yesu anatumia picha ambayo imezoeleka kwa wanao msikiliza-viriba
vipya na vya zamani. Kama ilivyo na muda maalumu wa kufunga na muda wa kufanya
sherehe, vile vile kuna muda wa zamani na muda mpya. Bwana wetu hataki sisi
tufungwe na mambo ya zamani tushindwe kuona na kukaribisha maisha mapya ya Roho
Mtakatifu katika maisha yetu. Anataka akili zetu na mioyo yetu viwe kama viriba
vipya-vilivyo funguliwa na kuwa tayari kupokea divai mpya inayowekwa ndani
yetu. Tambua kuwa anataka kuweka neema tele katika maisha yetu kama tutakubali
wenyewe kufanywa upya.
Sala: Bwana, natamani kuwa mpya. Natamani kuisha maisha mapya ya neema ili
neema tele ziweze kujazwa ndani mwangu zaidi kwa neno lako. Nisaidie Bwana
mpendwa, kukumbatia maisha mapya ya neema ulioweka ndani yangu. Yesu nakuamini
wewe. Amina
No comments:
Post a Comment