Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KATIKA SAFARI YA KUKUTANA NA YESU!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Januari 19, 2023
Juma la 2 la Mwaka wa Kanisa

Ebr 7:25 – 8:6;
Zab 40: 7-10;
Mk 3: 7-12


KATIKA SAFARI YA KUKUTANA NA YESU!


Somo la kwanza linatukumbusha kuhusu sadaka ya umilele ya Yesu. Makuhani wa Kilawi walikuwa wanarithiwa baada ya mmoja kufa. Lakini Yesu haitaji mtu wa kumrithi kwa sababu anaishi milele. Haitaji mtu wa kuchukua nafasi yake. Anaweza kuona kazi ya ukombozi ya watu wake kuanzia mwanzo hadi mwisho. Majaribu yetu hayapaswi kututenga na urithi wetu kwasababu Yesu anaendelea kutusaidia kwa huruma yake na neema yake, katika njia yetu mpaka tutakapo fikia mwisho. Ni faraja ilioje kutambua kuwa Yesu mwenyewe anatuombea kwa Baba kila wakati!

Katika Injili ya leo, inaelezea mapokeleo ya pekee aliopata Yesu. Tunaona watu wakisafiri kutoka umbali mrefu wakimtafuta Yesu. Walikuwa wamesikia habari zake na mambo aliokuwa akifanya. Haya yaliwafanya watu watembee umbali mrefu na kukutana naye wakiwa na Imani kubwa. Watu wanamtazama kama kiini cha mvuto wote. Alikuwa sehemu ya hija kwa watu hawa. Wahujaji wanasafiri wakitafuta uwepo wa Mungu au kuboresha imani waliokuwa nayo kabla. Safari inapambwa na kuwashwa na moto wa Imani, matamanio na matarajio. Kwa wahujaji mateso njiani sio kikwazo cha kuwazuia kwenda kumuona mtu waliotaka kwenda kumwangalia. Watu katika Injili wanao tembea kumtafuta ili wamsikilize Yesu ni msukumo kwetu sisi. Je, tupo tayari kutembea maili nyingi nakumtafuta Yesu? Je, nipo tayari kutembea mbele katika utakatifu na kuacha dhambi ambazo zinanifunga nishindwe kumuona Yesu na kumsikiliza?

Kama tumeamua kufanya hivyo, tunapaswa tufanye yafuatayo :

KUAMKA: Tunapaswa kuamka katika maanguko yetu ya kiroho. Hatuwezi kuendelea kutembea huku tumelala. Kwasababu wahujaji ni wale wanao tembea wakifahamu na kujitambua kuhusu safari yao.

KUACHIA: Tunapo anza safari yetu ya kukutana na Yesu, tunapaswa kuweka mizogo isio na maana ambayo itaturudisha nyuma tukiwa njiani.

KUTAZAMA: Wakati tukitembea katika njia yetu huku tukijaribiwa kurudi, tutazame mbele na kuwaona wahujaji waliokwisha tangulia na kufanikiwa.

KUJIJENGA: Kila hatua kumwelekea Yesu ni hatua ya kujenga uhusiano wetu naye na watu wengine. Katika safari hii, hatutembei wenyewe, bali tunatembea tukiwa na wengine.

Sala: Bwana, ninakushukuru kwa kunipa neema ya kukutana na wewe. Ninakushukuru kwa sadaka yako ya umilele uliotoa kwa ajili yangu. Ninaomba niamke kutoka katika usingizi wangu. Ninaomba nikutazame wewe pekee. Na ninaomba nijenge uhusiano wangu nawe. Yesu nakuamini wewe. Amina.


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment