“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Januari 24, 2023
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Fransisko wa Sales ( Askofu na Mwalimu wa Kanisa)
Ebr 10: 1-10;
Zab 40: 2-11;
Mk 3: 31-35
FAMILIA YA MUNGU!
Yesu aliongea mambo mengi yanayo stusha katika utume wake. Katika Injili ya
leo kuna aina Fulani ya ukimya unatawala katika umati wa watu wakati Yesu
alivyo ongelea kuhusu familia yake. Wengi waliomsikiliza kidogo walidhani Yesu
alimkosea heshima Mama yake na ndugu zake. Lakini je ni kweli? Je, unadhani
Mama yake alilichukulia hivi? Kwa hakika sio hivyo.
Hili linaonesha kwamba Mama yake zaidi ya wote, ndiye aliye yashika maneno
ya Mungu zaidi kuliko wote, na kwamba Mama yake alimtii Mungu na kufanya mapenzi
ya Mungu katika ukamilifu wote. Ndugu zake walikuwa muhimu. Lakini Mama yake
alikuwa zaidi, kwasababu alitimiza yote kwa utii mkamilifu katika kutii mapenzi
ya Mungu. Kwahiyo, kwa utii mkamilifu kwa Mungu, Maria alikuwa mama mkamilifu
wa Mwana wa Mungu.
Mara nyingine ujumbe wa Yesu hawakuuelewa. Kwanini hivi? Kwasababu Yesu
alijua ni kwa jinsi ghani ya kuwasilisha ujumbe wake na upokelewe vizuri.
Alijua ujumbe wake unaweza tu kupokelewa na wale wote waliofungua mioyo yao na
kwa Imani. Na alitambua wote walio fungua mioyo yao kwa Imani wataelewa au
kutafakari juu ya ujumbe wake mpaka utakapo ingia ndani kabisa. Ujumbe wa Yesu
hauwezi kuchukuliwa nakufanyiwa midahalo kama vile ni somo la falsafa. Maria
alisikiliza maneno hayo ya Yesu kwa Imani kamili alielewa na alijazwa na
furaha. Ilikuwa ni kwasababu ya “NDIO” yake kamili kwa Mungu iliyo mwezesha
kuelewa yote aliosema Yesu. Na pia hili lilimsaidia Maria kustahili jina
takatifu “Mama” zaidi ya kuwa na uhusiano wa damu. Uhusiano wake wa damu hauna
mashaka na nimuhimu, lakini la muhimu zaidi ni muunganiko wake wa kiroho ni
muhimu zaidi.
Sisi wote tunaitwa tujiunge kwa undani katika familia hii ya Yesu. Tunaitwa
kwenye familia yake kwa njia ya utii wetu wa kutii mapenzi ya Mungu. Tunaitwa
tuwe wasikivu, kusikiliza, kuelewa na kutenda yote anayotuambia Yesu. Tuseme
“Ndio” kwa Bwana wetu leo, na kuruhusu “Ndio” hiyo iwe ndio msingi wa kujiunga
na familia hii ya Mungu.
Sala: Bwana, nisaidie mimi daima niweze kukusikiliza kwa moyo uliofunguka.
Nisaidie niweze kutafakari juu ya maneno yako kwa Imani. Kwa tendo hili la
Imani, nisaidie mimi niweze kukuwa katika muunganiko nawe na kuingia katika
familia yako ya Kimungu. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment