“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatano, Januari 18, 2023
Juma la 2 la Mwaka wa Kanisa
Wiki ya kuombea umoja wa Wakrsito (Januari 18-25, 2023)
Ebr 7: 1-3, 15-17;
Zab 110: 1-4;
Mk 3: 1-6
DHAMBI INATIA MAWINGU MAISHA YETU!
Haiku chukuwa muda kwa Mafarisayo wivu juu ya Yesu kutanda fikra zao.
Mafarisayo walitaka watu wa waangalie na kuwaheshimu kama walimu waaminifu wa
sheria. Hivyo, Yesu alivyojionesha, na watu wakawa wanashangazwa na mamlaka
aliokuwa akifundisha nayo, mara moja Mafarisayo walianza kumpinga. Jambo la
huzuni ambalo tunaona katika matendo yao, ni kwamba, wanaonekana kuwa vipofu,
wivu ukiwajaa na kuwaweka mbali na ukweli kiasi kwamba wanashindwa wanafanya
kama watu wasiofikiri. Dhambi inatuchanganya sisi, hasa dhambi za ndani ya
roho, kama vile, majivuno, wivu na hasira. Na hivyo, mmoja anavyo chukuliwa na
moja ya dhambi hizi, mtu huyo hajitambui ni kwa jinsi ghani uwezo wa kufikiri
unavyopungua.
Yesu anawekwa katika hali ambayo anaamua kumponya mtu mmoja wakati wa
Sabato. Hili ni tendo la huruma. Linafanywa kwa mapendo ili mtu huyu aweze
kutoka katika mateso yake. Ingawaje huu ni muujiza wa pekee, akili za
mafarisayo zilizo tibuka wana angalia njia tu ya kubadili kitendo hiki cha
huruma kuwa kama kitendo kiovu. Sisi pia tunajitahidi katika hali moja au
nyingine, kwa dhambi kama hizi. Mwenzetu anatenda jambo jema, sisi tunajaribu
kulibadilisha na kutaka lionekane ni baya, kwa hofu ya kuogopa kupoteza
umaarufu wetu. Sisi pia tunajikuta tunaruhusu wivu na hasira kuingia ndani
mwetu na kuharibu hali yetu ya kuhusiana na wenzetu. Ni mara nyingi tumejikuta
tukihalalisha matendo yetu kama Mafarisayo wanalivyofanya. Tuchunguze maisha
yetu na tumwombe Yesu atuponye na kututakasa.
Nasi pia tunavyo anza oktava ya kuombea umoja wa Wakristo, tusijikute
tunawachukulia vibaya Wakristo wenzetu wasio wa Wakatoliki. Tuwe watu wa
kufanyaka kazi na kuomba kwa ajili ya umoja wa wakristo na umoja wa Kanisa.
Sala: Bwana Yesu, nisamehe mimi kwa dhambi zangu. Ninaomba msamaha na
ninasali ili niweze kuona yote yanayo funika uwezo wangu wa kufikiri na
kutenda. Niweke huru na unisaidie nikupende wewe na jirani zangu kwa upendo
mtakatifu ulio niitia. Yesu nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment