“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatatu, Desemba 2022
Juma la 4 la Majilio
Amu 13: 2-7, 24-25
Zab 70: 3-6, 16-17
Lk 1: 5-25
NITAKUWAJE NA HAKIKA?
Inavutia kulinganisha mazungumzo kati ya Zakaria
na Malaika Gabriel na yale ya Maria na Malaika Gabriel. Majibu yao kwa malaika
Gabrieli yanaonekana kuwa sawa, lakini Malaika Gabrieli anaonekana kumjibu kila
mtu kitofauti kabisa. Kwa Maria, malika Gabrieli anaelezea maelezo machache,
baada ya ombi la Maria la kutaka maelezo: “Hili linawezekanaje” Maria alisema.
Gabriel anajibu “Roho Mtakatifu atakufunika …..” lakini katika hali hii kwa
Zakaria hakutoa maelezo. Na badala yake Zakaria anakuwa bubu kwasababu ya
kushindwa kuamini. Ingawaje majibu ya Maria na Zakaria yanaweza kuonekana kama
yanafanana kwa kuangalia tu katika hali ya kawaida, ni Dhahiri kwamba mioyo yao
ilikuwa tofauti. Kwa Maria Mama Mbarikiwa, swali lake aliliuliza katika Imani
kamilifu. Alisikia Gabrieli akiongea akaamini. Lakini Imani huwa inatafuta
kuelewa, na ndivyo kwa Maria katika Imani timilifu, alitafuta kuelewa fumbo
ambalo linakuja kwake. Malaika Gabrieli anajibu kwa kumweleza kwa kifupi, na
Maria anafurahi kwa hilo..
Zakaria alimjibu Malaika, “nitajuaje hili?” kwa
maneno mengine, anakiri kutoelewa kama maneno haya yatakuwa kweli. Hivyo
alikuwa bubu, alama ya kwamba, kama huna Imani, hakuna chakusema.
Kila wakati Mungu anapojifunua kwetu, tunapaswa
kwanza kuamini, na kwa unyenyekevu mkubwa, tutafute ufafanuzi. Tufikirie juu ya
Imani yetu. Je, tupo tayari kutaka kuelewa na kukubali yote anayotaka
kutufunulia Mungu? Je, tupo tayari kukubali na kuamini anayo ongeo Mungu juu
yetu? Ingawaje mimi na wewe pengine hatupokei tena neno lake moja kwa moja
kupitia kwa malaika kwa kumuona kwa macho, tuna bahati ya kuwa na Mungu
akiongea nasi kwa njia ya Neno lake. Je, tunasikiliza na kujibu kwa Imani kama
Mama yetu Maria au Zakaria.
Sala: Bwana, ninaomba unipe moyo na Imani kama ya
Mama Bikira maria Mtakatifu. Japo, nakubali juu ya udhaifu wangu na dhambi
zangu, ninaomba kwa mfano wake na maombezi yake, nipokee kila siku neno lako
linalo hubiriwa kwetu. Ninaomba kila wakati niwe makini kwa neno lako na
kulipokea kwa moyo wa ukarimu. Yesu nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment