Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MATAMANIO YAKO YATAKATIFUZWE!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Desemba 24, 2022
Juma la 4 la Majilio

2 Sam 7: 1-5, 8-12, 14, 16;
Zab 88: 2-5, 27, 29;
Lk 1: 67-79


MATAMANIO YAKO YATAKATIFUZWE!


Jioni ya Kuzaliwa kwa Bwana Yesu, liturujia inatukumbusha sisi kuwa hakika Mungu anasikiliza sala zetu na anazitekeleza sala zote. Ndoto zetu zote na ndoto kubwa za kumuangalia muumbaji pia zinakamilishwa na Mungu. 

Katika somo la kwanza Mungu analikataa wazo la Daudi la kulijenga Hekalu la Bwana na alizitoa sababu tatu. Kwanza, hakukuwa na uhitaji kwani sanduku la agano lilihifadhiwa katika vibanda tokea Kutoka. Pili, Mungu hakuwaamuru watu wake wamjengee Yeye hekalu la kudumu. Tatu, Daudi alikuwa hastahili kulijenga hekalu kwasababu yeye alimwaga damu nyingi. Mungu alikuwa hamuadabishi Daudi wala kumkataa yeye bali alikuwa tu anaziongoza tena huduma zake. Alitakiwa awe kiongozi, sio mjenga hekalu.

Vile vile, daima Mungu haturuhusu sisi kuyachukua matamanio yetu. Wakati mwingine Yeye anafanya kutowezekana kwasababu anahitaji sisi tumtumikie Yeye katika njia nyingine. Utambuzi wa ukweli huu utawasadia wakristo wengi kujua yasiyo ya kweli na ndoto zakuogopesha.

Sala: Bwana, niongoze mimi katika njia Yako, maisha yangu kadiri ya mipango Yako. Amina.


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment