“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano, Desemba 21, 2022
Juma la 4 la Majilio
Wimb 2: 8-14;
Zab 33:2-3, 11-12, 20-21;
Lk 1: 39-45.
MAISHA YETU WIMBO WA FURAHA
Leo katika somo la kwanza kutoka katika kitabu
cha wimbo Uliobora, ni Wimbo wa shairi unaovutia kusikia na kuona. Wapendwa
wote wawili wanaimba kwa furaha juu ya furaha yao watakayo kuwa nayo watakapo
kuwa pamoja. Lakini lazima kusubiri. Muda bado. Injli ya leo ni kioo cha wimbo
wa upendo. Ni ujumbe wa upendo ambao unakuwa kati ya mama na mtoto aliyembeba.
Elizabeth alisubiri kwa miaka mingi kupata mtoto. Maria, msichana mdogo ana
miezi tu sio miaka ya kusubiri ili ahadi yake itimizwe. Salamu ya Maria, kuruka
kwa kichanga na wimbo wa Elizabeti unatangaza ukweli wa ahadi ya Mungu.
Ni rahisi kuona ukweli wa furaha ya Elizabeti
kutoka moyoni anavyo kutana na Mama wa Mungu na Bwana akiwa ndani ya tumbo la
Mama yake Maria. “Hii inakuwaje initokee mimi, hata Mama wa Bwana wangu
anitokee mimi”? Mstari huu unaonesha furaha ya kweli ya Elizabeth kukutana na
Maria na anaona tendo hili kuwa ni Baraka kubwa ya kukutana na Mama wa Mungu.
Ni dhahiri pia kwamba sio Elizabeth tu alifurahi bali hata Yohane Mbatizaji
aliyekuwa katika tumbo la Mama yake, anajazwa na furaha pia na anaruka kwa
furaha. Ni furaha ghani isio na kifani inayowatokea Elizabeth na mtoto wake
ambaye hajazaliwa bado. Je, tunafurahia uwepo wa Kristo anapokuja kwetu? Kama
Elizabethi na Mwanaye waliweza kuhisi uwepo wa Bwana, je, sisi hatuwezi kuhisi
uwepo wake? Tunapo ingia kanisani, je tunahisi uwepo wa Mungu mara moja? Je,
tunahisi utakatifu wake? Na tunapo mpokea Bwana katika komunyo takatifu
tunahisi uwepo wake? Je, mioyo yetu ipo tayari kumpokea tena Masiha anayekuja
kwetu? Hii inatakiwa kuwa na Imani na inachukuwa jicho ambalo limeelekezwa kwa
ujio wa uwepo wa Bwana. Noeli inapokaribia, sisi pamoja na wapendwa hawa, Maria
na Elzabeti tuimbe wimbo wa matarajio ya furaha.
Sala: Bwana, natamani kukuona wewe na kuku fahamu
wewe. Ninaomba nitambue uwepo wako kati yangu. Nisaidie mimi, niweze kuwa
makini hasa, katika uwepo wako katika komunyo takatifu. Ninaomba moyo wangu
uruke kwa furaha daima unapokuja kwangu katika hali hii kamilifu. Yesu,
nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment