Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

JE, UNATAKA KUWA SHAHIDI KWA YESU?


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Desemba 16, 2022
Juma la 3 la Majilio

Isa 56: 1-3, 6-8;
Zab 67: 2-8;
Yn 5: 33-36


JE, UNATAKA KUWA SHAHIDI KWA YESU?


Injili ya leo inasema kwamba, Yohane Mbatizaji alishuhudia ukweli. Alikuwa ni taa inayowaka na kungara ikitoa ushuhuda kwa mwanga wa ‘Yesu’. Yohane aliongea yote aliosikia kwa Baba (1:31-34) kuhusu Yesu, na alitoa ushuhuda kwa kweli, kweli ambayo ni Kristo. Mara ya kwanza Wayahudi walifurahia ushuhuda aliotoa Yohane kuhusu Yesu. Yohane alikuwa ni taa inayowaka iliotoa ushuhuda wa Umungu wa Yesu kama Masiha.

Kwa, wayahudi, ilikuwa kwanza kurudi kwa Yesu kwa mahubiri ya Yohane. Na ndipo waje kumwamini Yesu kwasababu ya ushuhuda mkubwa, kwa miujiza mikubwa aliofanya Yesu, kwa nguvu ya Neno lake na kwa ajili ya nguvu zake za kutakasa za uwepo wa Kimungu. Mara nyingi tunavutwa kwa Yesu kwasababu ya mahubiri na ushuhuda wa wenzetu. Na Yesu anatupa ushuhuda kwa miujiza yake anayotenda katika maisha yetu, kwa njia za Sakramenti za Kanisa, kwa njia ya neno la Mungu na kwa njia ya Ekaristi. Je, uwepo huu wa Yesu katika maisha yetu upo? Je, upo katika hali ya kuyumbayumba au katika hali ya uimara na undani kabisa? Je, imetusukuma sisi na kutubadilisha sisi au tumebaki bila kubadilika?

Tunaitwa leo tusiwe tu wafuasi wa Yesu bali pia tutoe ushuhuda wake kwa maisha yetu. Tunaitwa tutimize kazi kama ya Yohane Mbatizaji. Tujitafiti leo tupo wapi katika safari yetu ya Imani. Pengine tupo katika hali ya nafsi zetu tu, tunapaswa tukutane na Yesu katika hali ya ndani kabisa. Lakini pia tunapaswa kuwa mifano mizuri na ushuhuda kwa wengine wanaotaka kumfuata Kristo. Yesu anatutaka sisi tutoe ushuhuda wa kweli kwa watu wengine kuhusu yeye katika hali ya ndani kabisa. Tunaomba uwepo wake wa kimungu uwe kilele cha uelekezaji wa ushuhuda wa upendo wake na kutujali kwake.

Sala: Bwana, zamisha maisha yangu ya Imani yawe ya ndani kabisa. Ninapo kufuata kila siku naomba nisiridhike na hapa nilipo tu. Nisadie nikuruhusu wewe uongee na mimi katika hali ya ndani kabisa ya hali ya juu. Yesu nakuamini wewe. Amina
                                    

Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment