“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 25, 2022
SHEREHE YA KUZALIWA BWANA
Isa 52: 7-10;
Zab 98: 1-6;
Ebr 1:1-6;
Yn 1: 1-18
HURUMA IMEPATA KUWA HAI!
Huruma imepata kuwa hai na yenye kuonekana katika Yesu Mnazareti, na hata ikafikia kilele chake katika Yeye. Baba “aliye mwingi wa rehema” (Efe 2:4), baada ya kumfunulia Musa jina lake kuwa ni “Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli” (Kut 34:6), hakuwahi kuacha hata mara moja kuonyesha hali yake ya kimungu katika nafasi zote za historia. “Ulipowadia utimilifu wa wakati” (Gal 4:4), kila kitu kilipokuwa kimepangwa kadiri ya utaratibu wake wa ukombozi, alimtuma duniani Mwanae pekee ili kutufunulia upendo wake katika ukamilifu wake.
Leo Kanisa pamoja na viumbe vyote vyajawa na furaha kwani vimefanywa upya na kuwa kiumbe kipya kwa njia ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. “Neno” basi na uwe mwanga (Mwa. 1:3), lililoleta uumbaji sasa limeongelewa tena, kupitia kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mkombozi wetu. Mwanga (Yn. 1:8), sasa anang’ara katika giza. Mwanga, atoaye mwanga kwa kila mtu amekuja ulimwenguni. Mungu asiyefahamika, sasa amefanywa afahamike, Baba sasa anajidhihirisha mwenyewe, kupitia mwanae wa kiume, Yesu. Neno alifanyika mwili na akakaa kwetu.
Umwilisho au Noeli ni sherehekeo la furaha hii – Mungu wetu anakuwa mwili na anakuja kukaa ndani yetu wanadamu. Tukio hili liliufanya ulimwengu ufurahi , malaika walifurahi kwa Utukufu kwa Mungu, waliomba kwaajili ya amani duniani kwa watu. Ingawa ukaribisho wa Bwana Yesu haukuwa wa furaha sana ulimwenguni. Mkombozi hakuwa na nafasi ya kuzaliwa, bali katika uhakika, katika moja ya vijiji vidogo Bethlehemu. Hakuwa na tafrija ya ukaribisho, isipokuwa tu kwa baadhi ya wanyama katika hali ya ukimya na baadae wachungaji wachache waliomuabudu Yeye. Mfalme Herode alimchukulia mtoto kuwa kama ni tishio, alitaka mtoto Yesu auwawe. Katika miaka ya mbeleni, mkombozi wetu alikanwa, alivamiwa na kusulubiwa. Na kwa hayo yote aliyoyapokea, mkombozi pekee alirudisha huruma, huruma na upendo. Leo, Yesu amezaliwa kati yetu tena, katika hali yetu ya kumkana na hali ya dhambi; Yeye amezaliwa Bethlehemu ya hali ya ubinafsi, umimi, mateso, vita, unyonyaji, nakadhalika. Je, sisi tupo kama wachungaji, waliokwenda kwa Yesu na kuzitoa heshima zao au tupo kama Herode, aliyemchukua Yesu kuwa kama ni tishio la uhuru wetu, katika hangaiko la kutafuta starehe? Je, tunakwenda kufurahi pamoja na wachungaji au kupanga mabaya kama Herode?
Katika milongo miwili iliyopita, dunia yetu imekuwa nzuri sana kwa wanadamu pamoja na uwepo wa kimungu wa Mungu mwenyewe. Ndani yake pia, wengi wametamani kuwa katika giza. Kwa namna ya pekee, Yesu anahitaji azaliwe ndani yetu, awe Neno liletalo, mwanga unaoondoa giza lote, huruma inayo futa dhambi zetu. Je, tupo tayari kujitoa wenyewe kwake Yeye? Je, tupo tayari kuufahamu mwanga huo? Je, tupo tayari kupokea huruma yake?
Sala: Bwana Yesu, nakuhitaji Wewe uzaliwe ndani yangu leo, Nahitaji huruma yako inifanye chombo kikamilifu kwako. Ninahitaji kunena juu yako katika maneno na maisha yangu. Amina.
Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment