Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUMFAHAMU MUNGU KWA KUMPENDA JIRANI!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Desemba 29, 2022
Oktava ya Kuzaliwa Bwana.

1 Yoh 2: 3-11;
Zab 96: 1-3, 5-6;
Lk 2: 22-35.


 KUMFAHAMU MUNGU KWA KUMPENDA JIRANI!


Somo la kwanza la leo linaweka bayana kuwa tunaweza kumjua Mungu. Na njia pekee ya kumfahamu Mungu ni kwa kuziishi amri zake. Kumfahamu Mungu sio kwa vitendo, sio kwa akili au ufahamu wa kinadharia, bali ni wa mtu binafsi, mahusiano ya kimapendo. Hali ya Mungu kuwa mwanadamu ilikuwa na malengo mawili. Ilikuwa ni kuuleta ukombozi wa Mungu kwa kila mwanadamu, ambao Aliufanya kwa njia ya kuzaliwa kwa Yesu, kifo na ufufuko. Vilevile ilikuwa kudhihirisha Mungu ni nani, na mtu anayemuona Yesu, anamuona Mungu. Mwishoe kumfahamu Mungu kunawezekana tu kwa kuishi ndani ya Kristo, kuyaisha maisha yaliyo sawa na maisha ambayo Kristo aliyaishi. Kristo alimpenda kila mmoja, alizaliwa kwa ajili ya watu wote, aliishi na alikufa kwa ajili ya wengine. Kuishi ndani ya Kristo kunamaanisha kuwapenda ndugu zetu. Ukristo sio dini inayojikita kiini chake katika tamaduni na kuzitenda, bali ni njia ya maisha kwaajili ya mabadiliko ya kumrudia Mungu. Ni kama vile sisi hatuwezi kuwa tayari kumfahamu Mungu isipokuwa kwa kuwapenda wengine, hatutaweza kumuabudu Yeye, tusipokuwa na  upendo ndani yetu.

Sala: Bwana, nisaidie nikuige Wewe, ili niweze kumpenda kila mtu. Amina.


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment