“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Desemba 1, 2022
Juma la 1 la majilio
Isa. 26:1-6;
Zab 118:1,8-9,19-21,25-27;
Mt 7:21.24-27
NI KITU GHANI KINATUFANYA TUSITIKISIKE?
Leo tunasikia kuhusu wajenzi wawili, mmoja
anafanikiwa kwa kujenga nyumba yake juu ya mwamba, na mwingine anashindwa kwa
kujenga nyumba yake juu ya mchanga. Mjenzi wa kwanza anaweza kufananishwa na
mfuasi wa Kristo ambaye hasikilizi tu neno la Mungu nakuliacha bali analiishi
na kulitenda. Kwa upande mwingine, yule anaye sikia maneno ya Kristo, lakini
hayaweki katika matendo ni kama yule mjenzi wa pili aliyejenga nyumba yake
kwenye mchanga; kati yetu tumejenga nyumba nzuri kwa mwamba mzuri ili kujilinda
wenyewe na tufani mbali mbali, lakini je! Tumeandaa mioyo yetu ili kumpokea
Yesu wakati wa Noeli?
Ujumbe wa Injili upo wazi: kama tunataka kushinda
mawimbi na dhoruba za maisha na kubaki tukiwa tumesimama imara, tunapaswa
kuyaweka maneno ya Yesu ndani kabisa mwa mioyo yetu na kuyaweka katika matendo
yetu ya kila siku. Yesu ndiye mwamba imara pekee ambao tunaweza kuwa na tumaini
la kweli la kusimamia. Ni msingi wa jinsi tulivyo na yote tunayo tumaini. Ni
mwamba ambao Imani yetu imejengwa. Njia pekee ya kumwilisha neno la Mungu
katika maisha yetu, ni kusikia neno la Mungu kila wakati katika akili yetu
(kusoma neno la Mungu kila wakati). Ni kushibishwa na Neno.
Kipindi hiki cha majilio ni muda ambao tumepewa
na kanisa ili tuzame katika msingi wa maisha yetu ya kiroho kwa kusikiliza na
kutenda. Tunapo sikiliza, tunapaswa kutenda katika hali ya kumngojea Masiha
azaliwe katika mioyo yetu. Kwa njia hii, Noeli itasherekewa katika mioyo yetu
ilio simama imara na katika nyumba zetu.
Sala: Bwana, ninaomba maisha
yako ulioishi ya kibinadamu yawe msingi wa maisha yangu. Ninaomba maisha yangu
yajengwe ndani mwako wewe ambaye ni jiwe la msingi. Yesu, nakuamini. Amina
No comments:
Post a Comment