Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MFALME KATIKA UTAWALA WAKE


“MBEGU ZA UZIMA”
Jumapili, Novemba 20, 2022 
Juma la 34 la Mwaka C wa Kanisa

Sherehe ya Bwana wetu Yesu Kristo Mfalme

2 Sam 5:1-3;
Zab 121:1-5;
Kol 1:12-20;
Lk 23:35-43.


MFALME KATIKA UTAWALA WAKE. 

Hadithi moja ya Ireland, inaeleza wakati ambapo nchi ya Ireland ilitawaliwa na wafalme. Mflame aliyekuwa anatawala hakuwa na mtoto wa kuirithi enzi yake. Hivyo, aliwatuma wajumbe wake kutangaza ujumbe wake katika kila mji na kijiji cha utawala wake. Aliwaalika vijana waliohitimu kwa mkutano na Mfalme. Mfalme alihitaji sifa mbili: mtu lazima awe na upendo wa kina kwa Mungu na kwa jirani yake. 

Kijana mmoja alisikia tangazo hilo. Kwa hakika alikuwa na upendo wa dhati wa Mungu na kwa jirani. Lakini, alikuwa ni maskini sana, na hakuwa na mavazi ya adabu ya kuvaa katika mkutano na hakuwa na fedha za kununulia mahitaji muhimu kwa ajili ya safari ndefu kwenda kwenye ngome ya Mfalme. Aliamua kwenda kuomba nguo na mahitaji aliyotaka. Kila kitu kilipokuwa tayari, alianza safari yake. Baada ya mwezi mmoja wa safari, alifika karibu na ngome ya Mfalme, alimwona maskini mwombaji akikaa kando ya barabara. Mwombaji alinyanyua mikono yake juu akiomba msaada. “nina njaa na kujisikia baridi?” alisema kwa sauti ya kutetema, Je! unaweza kunipa kitu chochote nipate kula na nguo kuvaa? Kijana yule alivutwa sana na mwombaji. Alizitoa nguo zake za nje na kubadilishana na nguo za mwombaji zilizochakaa na kuchanika. Pia alimpatia mwombaji yule mahitaji aliyokuwa amebeba kwa ajili ya safari. Hii hairidhishi sana alitembea na nguo zilizochakaa kwenda kwenye ngome ya Mfalme. Alipofika kwenye ngome ya Mfalme, askari alimchukua kumpeleka eneo la wageni. Baada ya muda mrefu aliongozwa kwenda kumwona Mfalme. Aliinama kifudifudi mbele ya enzi ya Mfalme na aliponyanyua kichwa juu hakuweza kuamini macho yake. Alipomuona mfalme alimwambia: “Wewe ulikuwa ni mwombaji kando ya barabara!” Hakika ni kweli” alisema mfalme, “Nimetaka kujua zaidi kama hakika wampenda Mungu na jirani.” 

Hadithi hii hakika inalingana na liturujia ya leo. Mfalme wetu ni Mfalme mwenye Upendo. Anatupenda sisi bila kikomo kwamba yeye alikuwa tayari kutoa utukufu wake kutuokoa kutoka katika utumwa wetu wa dhambi. Ukweli alishuhudia Upendo. Je, sisi tunaweza kusikiliza sauti ya upendo wake. Je mambo yetu si juu juu kwake. Yeye ni Alfa na Omega wa Upendo. Toka kwake huanza upendo na pia kwake yeye upendo huishia kwa ukamilifu. Tukiwa wafuasi wa Kristo Mfalme tukumbuke kwamba mwishoni mwa maisha yetu, tutahukumiwa juu ya upendo pekee. Kwa hiyo, tunajaribu kuwa waaminifu kwa Ufalme wake wa Upendo. 

Kila tunapofikiria picha ya Mfalme, tunakumbushwa kuhusu kuvalishwa taji, au kuwa na utawala. Picha hizi zinaleta katika akili yetu alama ya fahari na utukufu wa Kifalme. Lakini tunavyo ona katika Injili ya leo Yesu anatangazwa kuwa Mfalme, akiwa na taji la miiba, taji la mti (msalaba) na ufalme wa wale waliomkataa na kumsulubisha. Je, ufalme na utukufu upo wapi? Kujibu hili, lazima tuwe na mawazo tofauti na ufalme tunao waza na Ufalme wa Yesu Kristo.

Tunapotafakari kuhusu Mfalme katika Agano la Kale, taswira na picha inayokuja kichwani ni kuhusu Mfalme Daudi. Katika somo la kwanza kutoka katika kitabu cha pili cha Samueli, tunasikia habari kuhusu kupakwa mafuta kwa Mfalme Daudi ili awe Mfalme juu ya Taifa la Israel. Tunaona kwamba Daudi alipata heshima na msaada kutoka katika makabila yote yaliokuwa chini yake. Tunaona katika utawala wake, taifa la Israeli likiingia katika kipindi cha neema, baada ya kuwashinda mataifa ya jirani waliokuwa wapinzani wao, na kuweza kuongeza utawala wao. Daudi aliwashinda Wapalestina maadui maarufu wa Waisraeli na hapo akajipatia umaarufu mkubwa kutoka kwa watu wake. 

Katika hali nyingine, tunapo ongolea kuhusu Ufalme wa Yesu mambo huwa kinyume na tofauti,  hata wafuasi wake walimtegemea aanzishe ufalme wa kisiasa kama ule wa Daudi hapa dunaini. Hapa ndipo tunapopaswa kufungua macho yetu, Yesu alikuja kuanzisha Ufalme wa Mungu sio ufalme wa kisasa au wa kuwa na mali ambao unaweza kuanguka na kuinuka, bali alikuja kuanzisha ufalme ambao utasimama imara milele. Kwa hiyo, mmoja anashiriki katika ufalme huu kikamilifu kwa njia ya ufufuko ambao alijishindia na kupewa kwetu na Mfalme wetu Bwana wetu Yesu Kristo. 

Utawala na utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo, upo juu zaidi ya ufalme wowote duniani kama inavyofunuliwa kwetu leo na somo la pili kutoka katika barua ya mtume Paulo kwa Wakolosai. Ingawaje ukamilifu wa ufalme wote utajulikana kabisa katika ujio wa pili wa Kristo, tayari alishausimika na kuanzisha ufalme huu kwa njia ya Ufufuko wake. Yesu aliishi nasi hapa duniani kama Mungu na mtu ili atuoneshe njia inayotupeleka kwenye ufalme wake. Utukufu wa Yesu unaonekana katika somo la pili, uliletwa na kudhihirika mara tu baada ya matokeo ya mateso yake pale msalabani, kifo na ufufuko.


Sala: Bwana Yesu Kristo, wewe ni Mfalme juu ya ulimwengu wote na nina tarajia ya kuwa wewe pekee ni Mfalme wa maisha yangu. Naomba unisadie niweze kukuona wewe kwa wale wenye njaa, na wanao ona kiu, kwa wagonjwa na wakimbizi niweze kukutumikia wewe. Amina


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment