“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Novemba 26, 2022
Juma la 34 la Mwaka wa Kanisa
Ufu 22:1-7;
Zab 94:1-7;
Lk 21:34-36
KUWA TAYARI NA SALI!
Siku ya leo masomo yanatualika kuwa tayari daima,
kuwa makini na pia kusali daima. Yesu leo anatupa ujumbe huo huo alivyo ulizwa
kuhusu ujio wa Ufalme wa Mungu (Lk 17:20-21). Ujio wa Ufalme wa Mungu utakuja
kama radi, bila kutegemewa, bila kuwa na kiashirio kabla. Tunapaswa kuwa makini
na kujiandaa. Kusubiri kukiwa kurefu sana, kuna hatari ya kujisahau na kupoteza
muelekeo. Yesu anatuonya hapa kwa vitu vitatu, kujikita kwenye anasa na kuwa na
ulafi, ulevi, na kusumbukia kwa kuwa na mashaka ya maisha haya. Tunapaswa kuwa
tayari na kuwa makini “ili siku hiyo isije ikatushika kama mtego”, ukumbusho
kwamba Mungu hapendi hata mmoja wetu apotee. Sala inatupa matumaini, inatufanya
tuwe tayari, inazima tamaa zetu na kutupa nguvu ya kuendelea kuishi katika neno
la Mungu. Inasaidia pia waamini kusimama tukiwa tumejiandaa mbele ya Mwana wa
Adamu.
Sala: Bwana, ninakupenda wewe Bwana na ninatamani kukupenda wewe zaidi ya yote. Nisaidie mimi niweze kusimama imara katika maisha yangu ya Imani. Nisaidie kukaza macho yangu kwako na kujiandaa utakapo kuja. Ninakuomba nijiandae kwa sala na fadhila, wakati nitakapo kutana na uso wako. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment