“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne, Novemba 29, 2022
Juma la I la Majilio
Isa 11:1-10;
Zab 71:1-2,7-8,12-13,17;
Lk 10:21-24.
KUWA MTOTO WA MUNGU!
Somo la kwanza linatufunulia kuhusu habari za
Masiha aliye jazwa Roho Mtakatifu na ambaye atakuwa kiongozi mkuu wa duniani na
mbinguni kama mtawala wa Amani. Yesu amesha kamilisha mpango wake, lakini sisi
tuliotokea kipindi Fulani bado tunapaswa kukubali wokovu wake aliotujalia.
Nabii katika somo la kwanza anatangaza wakati mpya, utakao anzishwa na Masiha.
Na hapo, alikuwa mfalme aliyetarajiwa, Yesu. Tunamuona yeye akiwa amejazwa na
Roho Mtakatifu akimtukuza Baba yake kwasababu ya ushindi mkubwa dhidi ya muovu
shetani. Ushindi huu wanaushinda pia wafuasi wake, wale sabini walifurahi
kwasababu walimuona shetani akishindwa (Lk 10: 1-17). Hii ni akili waliopewa
wafuasi na Kristo-kwamba Mungu ametukomboa sisi kutoka kwenye dhambi, kifo na
maovu yote. Wafuasi wanarudi kutoka katika safari yao ya kwanza ya kimisionari.
Wanafurahi “hata shetani anakimbia kwa jina lako Bwana” Yesu anamshukuru Baba
yake kwa kuwafunulia mambo haya watu hawa wakawaida, na sio wale walio
mashuhuri na werevu wa akili wa dunia hii. Yesu anawaita wafuasi wake “watoto
wachanga”.
Je, watoto ni akina nani? Ni wale sabini walio
rudi kutoka kutoka katika utume., watu wa akawaida wasio na elimu kubwa, lakini
walio msadiki Mungu. Kwahiyo kama tunataka kuelewa vitu vya Ufalme wa Mungu,
tunapaswa kuwa wafuasi, wadogo kabisa! Udogo unamaanisha matendo ya Ufalme
katika mambo yetu ya kawaida ya maisha. Wafuasi walihisi zawadi hii ya Mungu
walio liita jina la Yesu katika mahubiri yao na kuponya. Leo, Yesu anatuita
katika uhusiano naye wa karibu na Pia na Baba yake. Anatuita ‘Rafiki”, sio
watumwa” kwasababu ametueleza yote kuhusu yeye; na anatuambia tumuite Mungu
“Baba yetu” kama yeye alivyokuwa akimwita.
Sala: Bwana, nipe moyo wa
udogo na mnyenyekevu na imani kama ya mtoto. Nisaidie niweze kukuona wewe kama
ulivyo, na kuruhusu uwepo wako duniani uingie katika maisha yangu. Yesu,
nakuamini. Amina.
No comments:
Post a Comment