“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne,
Oktoba 11, 2022
Juma
la 28 la Mwaka wa Kanisa
Gal
5:1-6
Zab
118:41, 44-45, 47-48
Lk
11:37-41
YESU
ANAYASEMA YOTE KWA UWAZI
Mafarisayo
walijivuna nakujiona wao wenyewe kuwa wema na wasafi kwa kushika mapokeo na
sheria. Waliigawa jamii katika makundi ya walio wema na walio wabaya, wakijiona
wenyewe kuwa wema na watu wamataifa mengine kuwa waovu. Kwa njia ya taratibu na
sheria zilizo tengenezwa na wanadamu walifunga ufalme wa Mungu kwa watu wa
mataifa mengine (waliodhani ni waovu). Walijifanya kuonekana wasafi na wema
kumbe mioyo yao ilikuwa minafiki na miovu. Yesu anaonya juu ya unafiki wao wa
kila wakati.
Mungu
anaisoma mioyo ya watu. Kama ndani ya mtu ni giza, mwili wote unakuwa giza na
mtu hawezi kujidai ni mtu wa Mungu. Yesu anatoa ujumbe mkubwa kabisa kwa wote,
hasa kwa viongozi wa dini, wawe watu wa Mungu kweli, wenye tabia za Kimungu,
utu na maadili mema. Ni mtu mzuri tu anayeweza kuzaa matunda mema ya roho,
ambayo ni , “upendo, furaha, Amani, upole na kujitawala” (Gal 5:22 – 23).
Katika
Injili tunamuona Mfarisayo anamualika Yesu kwa chakula. Yesu alifahamu lengo la
Mfarisayo kumualika kwa chakula cha pamoja. Walitaka kutafuta kosa ili
wamhukumu Yesu. Lakini Yesu anachukua nafasi hii kurekebisha mawazo yao. Yesu
alikuwa mtu mwazi. Alienda kwa chakula cha pamoja na akawarekebisha. Sisi nasi
tuna nafasi mbali mbali za kuwarekebisha watu wengi tunaokutana nao katika
maisha yetu. Je, tupo tayari kusema ukweli kwa ajili ya kuleta marekebisho mema
na kutokomeza uovu? Au tunasubiri mpaka mtu akosee ili tufurahi na ndipo
tunapoenda kumweleza ukweli? Je, matendo yangu katika dini yangu yananifanya
niwe chombo cha Amani na umoja katika jamii ninayoishi?
Sala:
Bwana, tufanye waaminifu na wakweli. Tupe utambuzi wa unafiki wowote mahali
popote, lakini usituache tusahau unafiki wetu wenyewe. Tusaidie tuweze kutambua
kuwa mabadiliko haya kama mengine yanapaswa yaanzie ndani maana yake ndani ya
mioyo yetu na akili zetu. Amina.
Copyright
©2013-20226 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment