MASOMO
YA MISA, OKTOBA 11, 2022
JUMANNE,
JUMA LA 28 LA MWAKA
SOMO
1
Gal 5:1-6
Maana
katika kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno,wala kutotahiriwa,bali Imani
itendayo kazi kwa upendo.
Somo katika waraka wa mtume Paulo kwa
wagalatia.
Katika
ungwana huo kristo alituandikia huru kwa hiyo simameni wala msinaswe tena chini
ya kongwa la utumwa. Tazama mimi Paulo nawambia ninyi ya kwamba mkitahiriwa,
Kristo hatawafaidia neno. Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye,kwamba ni
wajibu wake kutimiza torati yote.Mmetengwa na kristo mtakao kuhesabiwa haki kwa
sheria ; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa roho
tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya Imani.Maana katika Kristo Yesu
kutahiriwa hakufai neno,wala kutotahiriwa , bali Imani itendayo kazi kwa
upendo.
Hilo
ndilo neno la Bwana… Tumshukuru Mungu
WIMBO
WA KATIKATI
Zab
119:41,43-45,47-48
(K)
Ee bwana fadhili zako zinifikie na mimi
Ee
bwana fadhili zako zinifikie na mimi
Naam
wokovu wako sawasawa na ahadi yako
Nami
nitamjibu neno anilaumuye
Kwa
maana nalitumainia neno lako (K)
Nami
nitaitii milele na milele
Naam
milele na milele
Nami
nitakwenda panapo nafasi
Kwa
kuwa nimejifunza mahusia yako (K)
Nami
nitajifurahisha sana kwa maagizo yako
Ambayo
nimeyapenda
Na
mikono yangu nitayainulia
Maagizo
yako niliyoyapenda
Nami
nitazitafakari amri zako. (K)
SHANGILIO
Zab
119:135
Aleluya ,aleluya,
Umwangazie
mtumishi wako uso wako,
Na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
INJILI
Lk.
11:37-41
Yesu
alipokuwa akinena, Farisayo mmoja alimwita aje kwake ale chakula; akaingia,
akaketi chakulani. Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa
kabla ya chakula. Bwana akamwambia, Ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na
sahani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyang’anyi na uovu. Enyi wapumbavu;
aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndania pia? Lakini, toeni
sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture
readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by
T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible
Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment