MASOMO
YA MISA, OKTOBA 6, 2022
ALHAMISI,
JUMA LA 27 LA MWAKA WA KANISA
SOMO 1
Gal.
3:1 – 5
Enyi
Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa
wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja
kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na
Imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka
kukamilishwa sasa katika mwili? Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure?
Ikiwa ni bure kweli. Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je!
Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na Imani?
Neno la
Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WAKATIKATI
Lk.
1:69 – 75 (K) 68
(K)
Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake.
Ametusimamishia
pembe ya wokovu
Katika
mlango wa Daudi, mtumishi wake.
Kama
alivyosema tangu mwanzo
Kinywa
cha manabii wake watakatifu. (K)
Tuokolewe
na adui zetu
Na
mikononi mwao wote wanaotuchukia;
Ili
kuwatendea rehema baba zetu,
Na
kulikumbu agano lake takatifu. (K)
Uapo
aliomwapia Ibrahimu, baba yeu,
Ya
kwamba atatujalia sisi,
Tuokoke
mikononi mwa adui zetu,
Na
kumwabudu pasipo hofu,
Kwa
utakatifu na kwa haki
Mbele
zake siku zetu zote. (K)
SHANGILIO
1Per.
1:25
Aleluya,
aleluya,
Neno la
Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
11:5-13
Yesu
aliwaambia wafuasi wake: Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa
manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu rafiki
yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; na
yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi
tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe? Nawaambia ya
kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile
asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
Nami
nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nayi
mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye
abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba
mkate, atampa jiwe? Au samaki, badala y asamaki atampa nyoka? Au akimwomba yai,
atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa
vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao
wamwombao?
Neno la
Bwana… sifa kwako Ee Kristu.
Copyright
© 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture
readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by
T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible
Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment