“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi,
Oktoba 6, 2022
Juma la
27 la Mwaka wa Kanisa
Gal 3:
1-5;
Lk 1:
69-75;
Lk 11:
5-13
KUOMBA!
“Ombeni
nanyi mtapewa…” nimeomba mara nyingi, lakini sikupata hata kimoja. Haya ni
majibu yetu kila mara kwenye huo ujumbe katika Injili. Lakini tujiulize,
tunatulia nakujitafiti na kutafakari; je, nimeomba kwa ajili ya malengo sahihi?
Je, ninafahamu thamani ya vitu ninavyo omba? Je, vitu ninavyo omba na kuhitaji
nivya lazima kabisa? Mtoto asiye na meno anaweza kumuomba baba yake mua. Je,
baba yake atampa? Hapana. Baba atasubiri mpaka akue awe na meno ndio ampe.
Nyani hafahamu thamani ya dhahabu ulioshika. Lakini aweza kunyosha mkono
kuomba, je utampatia? Hapana, haumpi. Kwasababu unafahamu thamani yake! Ni
katika hali hiyo tunaweza tusijue tunanyoosha mkono kuomba nini, lakini Mungu
anajua. Hii haimanishi tusiombe chochote tunacho penda. Tunaweza kuomba lakini
kama hatuvipati tunavyo omba, tusikatishwe tamaa. Mungu anajibu katika hali
ambayo itakunufaisha na njia ambayo itakufanya ulicho omba kisikutenge naye.
Sala:
Bwana, naomba mapenzi yako yatendeke. Amina
Copyright
©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment