Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, OKTOBA 31, 2022


MASOMO YA MISA, OKTOBA 31, 2022
JUMATATU, JUMA LA 31 LA MWAKA WA KANISA

SOMO 1
Flp. 2:1 – 4

Ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyoe na rehema, ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo yaw engine.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 131

(K) Moyo wangu uwe na amani kwako, Ee Bwana.

Bwana, moyo wangu hauna kiburi,
Wala macho yangu hayainuki.
Wala sijushughulishi na mambo makuu,
Wala na mambo yashindayo nguvu zangu. (K)

Hakika nimeituliza nafsi yangu,
Na kuinyamazisha.
Kama mtoto aliyeachishwa
Kifuani mwam mama yake;
Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu. (K)

Ee Israeli, umtarajie Bwana,
Tangu leo na hata milele. (K)

SHANGILIO
Zab. 130:5

Aleluya, aleluya,
Roho yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.

INJILI
Lk. 14:12 – 14

Yesu alimwambia yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.                        

No comments:

Post a Comment