Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUTEMBEA KATIKA NJIA WASIO SAFIRI MARA KWA MARA


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatatu, Oktoba 31, 2022
Juma la 31 la mwaka wa Kanisa

Flp 2:1-4;
Zab 130:1-3;
Lk 14:12-14,


KUTEMBEA KATIKA NJIA WASIO SAFIRI MARA KWA MARA!

Somo la Injili la leo linatuangaza sisi kuwanyanyua maskini na wale waliotengwa kama wafuasi wa Kristo. Luka leo anaelezea tukio ambalo Yesu alialikwa na mmoja wa fariso kwa chakula cha jioni. Katika kipindi cha Yesu ilikuwa kawaida watu kuwa alika marafiki, ndugu na jamaa kwa chakula. Hakuna ambaye angeweza kukaa mezani na mtu asiyemfahamu. Walikaa mezani na wale tu walio wafahamu na marafiki. Yesu hafurahishwi na hali hii au utamaduni huu wa watu. Anawaalika kuvunja hali hizo za kualika watu wa karibu tu, na badala yake wawa alike pia: maskini, viwete, waliotengwa na vipofu. Yesu kwakufanya hivi anatuongoza kwenye Baraka: “Mtabarikiwa kwasababu hawana cha kuwalipa”. Tunapaswa kufanya hivi bila kuwa na mambo binafsi na hofu ya watu ili tuweze kupata Baraka hii. Yesu anaikumbusha jamii pia kuvuka viwango vyao vya kujiwekea mipaka na badala yake kuhubiri Injili ya upendo.

Sala: Tusaidie Bwana, tufanyae ulichosema, hata ikiwa kinaenda kinyume na tamaduni zetu. Amina.


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment