MASOMO
YA MISA, OKTOBA 10, 2022
JUMATATU,
JUMA LA 28 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
LA 1
Gal 4:22-24, 26-27, 31:5:1
Imeandikwa
ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili.Mmoja alikuwa mjakazi na mwingine
alikuwa muungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa
muungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama
maagano mawili, mmoja kutoka Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni hajiri. Bali
Yerusalemu wa juu ni mwungwana naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa,
furahi wewe uliye tasa, usiye zaa; paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu:maana
watoto wakealiyeachwa pekee ni wengi kuliko huyo aliye na mume. Ndiposa, ndugu
zangu, sisi si watoto wa mjakazibali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.
Katika ungwana huo Kristo alituandikia huru;
kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Neno
la Bwana... Tumshukuru Mungu
WIMBO
WA KATIKATI
Zab
113:1-7 (K) 2
Aleluya
Enyi
watumishi wa Bwana sifuni
Lisifuni
jina la Bwana
Jina
la Bwana lihimidiwe
Tangu
leo na hata milele. (K)
(K)
Jina la Bwana lihimidiwe milele
Toka
mawio ya jua hata machweo yake
Jina la bwana husifiwa
Bwana
ni mkuu juu ya mataifa yote
Na
utukufu wake ni juu ya mbingu (K)
Ni
nani aliye mfano wa bwana
Mungu
wetu aketiye juu
Anyenyekeaye
kutazama
Mbinguni
na duniani?
Humwinua
mnyonge kutoka mavumbini
Na
kumpandisha masikini toka jaani. (K)
SHANGILIO
Zab
119:34
Aleluya, aleluya
Unifahamishe
nami nitaishika sheria yako
Nitaitii kwa moyo wangu wote
Aleluya
INJILI
Lk.
11:29-32
Makutano
walipokuwa wakimkusanyikia, Yesu alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya;
kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona. Maana, kama vile
Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa
kizazi hiki. Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi
hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka nchi za
dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani. Watu wa
Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa
na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa
kuliko Yona.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright
© 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture
readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by
T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible
Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment