“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa,
Oktoba 14, 2022
Juma
la 28 la Mwaka wa Kanisa
Ef
1:11-14;
Zab
32:1-2, 4-5, 12-13;
Lk
12:1-7
KUTANGAZA
INJILI BILA WOGA!
Je,
inakusumbua kuhusu wengine wana waza nini juu yako? Kwa namna unavyo vaa? Kwa
namna unavyosema? Je, unashindwa kufanya kitu flani au kutokufanya kwasababu
mtu flani atafikiri je? Hii ndio hofu ya mwanadamu na hii sio hofu sahihi. Hofu
sahihi ni hofu ya Mungu, kuhusu anachofikiri na anacho tuamuru, na nini anacho
tegemea. Lakini sio kwa hofu kama ya mtu anaye adhibu. Hofu ya mwamini ni
heshima kwa Mungu. Hofu hii ni msukumo wetu wakujikabidhi kwa Muumbaji wa
ulimwengu. Ambaye ni Mungu.
Katika
Injili ni mwaliko wa kuwa bila hofu na hasa wakati wa majaribu na mateso.
Mkristo hapaswi kuwa na hofu anavyo hubiri Injili ya upendo, ndio, hata katika
mapaa ya nyumbani. Ili kuhubiri huku kuwe na matunda kamili, Mungu amesia ndani
mwetu na kututia mafuta kwa Roho Mtakatifu (Ef 1:13; 2Kor 1:21) kama kusimikwa
kwetu kwanza kwa ajili ya safari ya wokovu wetu. Hatujapokea roho wa utumwa wa
kutupeleka kwenye hofu, bali Roho wa Mwana ambaye kwa njia yake tunalia ‘Abba
Baba” (Warumi 8:15). Kwa ajili ya kuhubiri kusiko na hofu, na sio kuanguka
kwenye hofu na ni vizuri kwamba tukuwe katika Roho Mtakatifu.
Sala:
Bwana, tusaidie tuweze kutenda kwa kadiri wa Roho asiye na hofu, ambaye
umetuita kuhubiri katika Injili. Amina.
No comments:
Post a Comment