“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi,
Oktoba 17, 2024
Juma
la 28 la Mwaka wa Kanisa
Ef
1:1-10;
Zab
97:1-6;
Lk
11:47-54
JE
TUNA UPANA WA AKILI KATIKA MAISHA YETU?
Injili
ya leo inaongelea kuhusu kutokuelewana kati ya Yesu na viongozi wa dini wa
wakati huo. Walimu washeria walimwelezea Mungu kama hakimu mkali sana na
wakaweka sheria na miiko ambazo hazikuwa na ushusiano kabisa na amri za Mungu.
Wao kwa njia ya mafundisho ya uongo waliwahukumu na kuwaua Manabii, na baadaye
walitengeneza makaburi kwa heshima yao. Leo Yesu anawanyoshea kidole, kwamba
wanajizuia wenyewe nakujiwia mizigo katika kuingia Ufalme wa Mungu na pia kuua
hamu ya wengine ya kumtumikia Mungu.
Swali
ambalo tunaweza kujiuliza wenyewe:
•
Je, tuna sura ya uongo ya Mungu na tunajaribu kuiweka kwa wengine?
•
Je, tuna upana mdogo wa uwelewa kama Waandishi ambao waliwapinga wengine
kwasababu tu, wanafikiri tofauti na kutenda tofauti?
Sala:
Bwana, naomba utupilie mbali mawazo yote mabaya na mitazamo yote mibaya
inayonizuia kujikabidhi kwangu kwako, mimi na jirani yangu, nisaidie niweze
kuwa na upana wa akili katika kukuelewa wewe katika jamii na jumuiya yangu.
Amina.
Copyright
©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment