Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MUNGU YUPO NASI KATIKA MATESO!



“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne, Oktoba 1, 2024 
Juma la 26 la Mwaka


KUMBUKUMBU YA MT. TERESIA WA MTOTO YESU

Ayu 3:1-3, 11-17, 20-23
Zab 88: 2-8
Lk 9: 51-56


MUNGU YUPO NASI KATIKA MATESO!


Ayubu anawakilisha maswali yote makubwa makubwa tunayo uliza… 

“Ni nini maana ya maisha ya mtu?” 
“Kwa nini mimi nipo hapa?” 
“Je, nina hitaji majukumu haya?” 
“Kwa nini mimi, Mungu?”

Somo la kwanza leo linamfanya mtu achunguze lengo la maisha yake, yana thamani ipi, mwisho ni upi, na umuhimu wake. Huwa tunatazama huku na huku na tunashangaa kwanini watu wanatenda kama wanavyotenda na kwanini wanafanya maamuzi hayo. Ni nini thamani ya nguvu, utajiri, tamaa yake na kwa uzuri ghani?

Somo linasema wazi kwamba “Mbona yeye aliye mashakani kupewa mwanga, na hao wenye uchungu rohoni kupewa uhai? Lakini bado, kama sio kwa mwanga na mngao wa matumini ingewezekanaje hata mmoja wetu kuenenda katika ulimwengu huu? Walio katika maisha, wanao ogopa maisha na wanao limbikiza hofu kwenye maisha ya wengine, wanao shindwa kuupata mwanga/uzuri/utajiri uliojificha kwa wengine na katika mazingira ya maisha.

Mungu anatualika tufungue mioyo yetu, ili tuone uzuri wake unao tuzunguka na kukumbatia uzuri huo. Tutakaposhindwa kuuona “utajiri uliofichika”, uzuri katika hali zetu na uzuri katika mazingira, mwanga wa njia hatutauona. Mungu anaendelea kutukusanya kwake, ili tuweze kuona wingi wa uzuri wa maisha haya, upendo wa Mungu kwa ajili yetu na tamaa ya Mungu ya kupenda sisi tushiriki naye maisha ya umilele.

Injili ya Luka leo, inanikumbusha kwamba, kwasababu tu watu hawaendani au hawakidhi viwango vyangu haimanishi tupaswa kuwahukumu. Mungu ametuumba sisi wote kama kiumbe pekee tulio na kazi ya kutimiza katika maisha. Pengine watu wa kijiji cha Samaria hawakuwa watu waliojali ujio wa Yesu, lakini kijiji kingine walichukua nafasi yao na kumjali. Hatupaswi kukata tamaa wakati maisha yanavyo “enda kinyume na mapenzi yetu”- bali tunapaswa kubaki katika uhusiano na Mungu kila mara, na kuamini kwamba kila tukio linatokea kwa lengo fulani. Tunapaswa kuwa watu wa sala na matumaini tusio na hofu na badala yake kuamini kwamba Mungu atatuongoza kwenye malengo yetu.

Sala: Bwana, ninaomba niweze kuona uwepo wako kila mara katika hali zangu ngumu za maisha kila wakati. Ili kwa matumaini makubwa niweze kuona utendaji wako wa ajabu katika maisha yangu. Amina


Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment