JUMANNE, OKTOBA 01, 2024
JUMA LA 26 LA MWAKA
KUMBUKUMBU YA MT. TERESIA WA MTOTO YESU
SOMO 1
Ayu. 3:1 – 3, 11 – 17, 20 – 23
Ayubu alifunua kinywa chake, na kuilaani siku yake. Ayubu akajibu, na kusema; naipotee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, na ule usiku uliosema, mtoto mume ametungishwa mimba. Mbona sikufa mimi tokea mimbani? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni? Mbona hayo magoti kunipokea, au hayo maziwa, hata nikanyonya, maana hapo ningelala na kutulia; ningelala usingizi; na kupata kupumzika; pamoja na wafalme na washauri wa dunia, hao waliojijengea maganjoni; au pamoja na wakuu wenye dhahabu, waliozijaza fedha nyumba zao; au, kama kuzikwa mimba iliyoharibika, nisingekuwako; kama wachanga wasiouona mwanga kabisa.
Huko waovu huacha kusumbua; huko nako hao waliochoka wakapumzika. Mbona yeye aliye mashakani kupewa mwanga, na hao wenye uchungu rohoni kupewa uhai; ambao wangojea mauti, lakini hawayapati; na kuyachimbulia zaidi ya kutafuta hazina iliyositirika; ambao wafurahi mno, na kushangilia watakapoliona kaburi? Kwa nini mtu aliyezibiwa njia kupewa mwanga, ambaye Mungu amemzingira kwa ukigo?
Neno la Bwana ..................Tumshukuru Mungu
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 88:1 – 7 (K) 2
(K) Maombi yangu yafike mbele zako, Ee Bwana.
Bwana, Mungu wa wokovu wangu,
Mchana na usiku nimelia mbele zako.
Maombo yangu yafike mbele zako,
Uutegee ukulele wangu sikio lako. (K)
Maana nafsi yangu imeshiba taabu,
Na uhai wangu umekaribia kuzimu.
Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni,
Nimekuwa kama mtu asiye na msaada. (K)
Miongoni mwao waliokufa nimetupwa,
Kama waliouawa walalao makaburini.
Hao ambao Wewe huwakumbuki tena,
Wametengwa mbali na mkono wako. (K)
Mimi umenilaza katika shimo la chini,
Katika mahali penye giza vilindini.
Ghadhabu yako imenilemea
Umenitesa kwa mawimbi yako yote. (K)
SHANGILIO
Zab. 130:5
Aleluya, aleluya,
Roho yangu inamngoja Bwana,
na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.
INJILI
Lk. 9:51 – 56
Ilikuwa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, Yesu aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu; akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. Wanafunzi wake Yakobo na Yohane walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize? Akawageukia akawakanya, wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment