Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, JUMANNE, AGOSTI 2, 2022



MASOMO YA MISA, 
JUMANNE, AGOSTI 2, 2022
JUMA LA 18 LA MWAKA


SOMO 1
Yer. 30:1 – 2, 12 -15, 18 – 22

Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia.

Maana Bwana asema hivi, Maumivu yako haya ponyekani, na jeraha yako ni kubwa. Hapana mtu wa kukutetea; kwa jereaha yako huna dawa ziponyazo. Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jereha ya adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu ya dhambi zako zilikuwa zimeongezeka. Mbona unalilia maumivu yako? Hayaponyeki maumivu yako; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zimeongezeka, nimekutenda haya.

Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa na kuyahurumia makosa yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyo desturi yake. Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; name nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge. Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko litathibitika mbele zangu, name nitawaadhibu wote wawaoneao. Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema Bwana.

Nayi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.



WIMBO WA KATIKATI
Zab. 102: 15 – 20, 28, 21 – 22 (K) 16

(K) Bwana atakao kuwa ameijenga Sayuni, atakapoonekana katika utukufu wake.

Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana,
Na wafalme wote wa dunia utukufu wako;
Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana katika utukufu wake,
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau maombi yao. (K)

Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo,
Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi,
Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na kuwafungua walioandikiwa kufa. (K)

Wana wa watumishi wako watakaa,
Na wazao wao wataimarishwa mbele zako. 
Watu walitangaze jina la Bwana katika Sayuni,
Na sifa zake katika Yerusalemu,
Pindi mataifa watakapokusanyika pamoja,
Falme nazo ili kumtumikia Bwana. (K)



SHANGILIO
Zab. 27:11

Aleluya, aleluya,
Ee Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.



INJILI
Mt. 14:22 – 36

Yesu alipowalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.

Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mara Yesu akanena, akawaambia, Jipeni moyo; ni mimi; msiogope. Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye Imani haba, mbona uliona shaka? Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma. Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.

Na walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti. Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi; nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa kabisa.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo


Copyright © 2022 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment