“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne, Agosti 2, 2022,
Juma la 18 la Mwaka
Yer 30:1-2, 12-15, 18-22;
Zab 101:16-23, 29;
Mt 14: 22-36.
KUFANYA YASIOWEZEKANA!
Petro alikuwa mvuvi aliyebobea na aliijua bahari vizuri sana. Lakini leo Petro anaambiwa afanye jambo lililo juu zaidi ya utaalamu wake-kutembea juu ya maji. “Yesu aliwaamuru wanafunzi wake wapande mashua wamtangulie ng’ambo ya ziwa”, alijua ya kuwa hali ya bahari sio shwari, wakati mwingine Yesu anaweza kuacha tukumbwe na changamoto au tupitie sehemu ngumu lakini ana sababu yake. Ili kutembea kwenye maji, Petro alihitaji kutoka nnjee ya mashua. Wakati Yesu anatutaka tufanye mambo ya hali ya juu anatutaka sisi tutoke nnjee ya hali ya sasa ili tuweze kufanya tendo lililo jaa Imani, matendo ya ajabu. Tusipokuwa na ujasiri wakutoka nnjee ya mashua zetu na kumuamini Yesu, hawezi kufanya kitu kwetu. Tutoke njee ya ubinafsi na hali zote zisizo mpendeza Mungu ili tukutane na Yesu, tukisha kutana naye tuwe na Imani na muelekeo wetu uwe kwake, tusiwe na mashaka na wasiwasi tusije tukazama, tusiyumbishwe na mawimbi bali tujishike naye daima yeye atafanya bahari ya maisha kuwa shwari na tulivu. Kwa hiyo, tuwe tayari kutembea na Yesu katika bahari ya maisha.
Sala: Nipo tayari kufuata amri zako Ee Bwana. Amina
Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment