Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, JULAI 01, 2026

 



MASOMO YA MISA, JULAI 01, 2026
JUMATANO, JUMA LA  13 LA MWAKA WA KANISA


SOMO 1
Amo. 5 : 14-15,21-24

Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo Bwana, Mungu wa majeshi, aiakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo. Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba Bwana, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.

Mimi nazichukia sikukuu zenu, asema Bwana nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini. Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona. Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu. Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama maji makuu.


WIMBO WA KATIKATI
Zab. 50 : 7-13, 16-17 (K) 23

(K) Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.

Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena,
Mimi nitakushuhudia, Israeli;
Mimi ndimi niliye Mungu, Mungu wako. (K)

Sitakukemca kwa ajili ya dhabihu zako,
Na kafara zako ziko mbelc zangu daimu.
Wala beberu katika mazizi yako. (K)

Maana kila hayawani ni wangu.
Na makundi juu ya milima eltu.
Nawajua ndege wote wa milima,
Na wanyama wote wa mashamba ni wangu. (K)


Kama ningekuwa na njaa singekuambia
Maana ulimwengu ni wangu, navyo viujazavyo.
Je! Nile nyama ya mafahali!
Au ninywe damu ya mbuzi! (K)

Maana wewe umechukia maonyo,
na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. (K)


SHANGILIO
2 Kor. 5 :19

Aleluya, aleluya, Mungu alikuwa ndani ya Kristu, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, ametia ndani yetu neno la upatanisho. Aleluya.


INJILI
Mt. 8 :28-34

Yesu alipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja Kututesa kabla ya muhula wetu?

Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe. Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini. Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote, na habari za wale wenye pepo pia. Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao.



Copyright © 2026 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published. These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment