“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Mei, 28, 2026,
Juma la 8 la Mwaka
1Pet 2: 2-5, 9-12;
Zab 100:2-5;
Mk 10:46-52.
KUONA TENA!
Leo, wakati Yesu akiuacha mji, akiwa anafuatana na wafuasi wake na umati mkubwa wa watu, kulikuwa na kipofu mmoja muombaji anayeitwa Batimayo mwana wa Timayo, akiwa amekaa pembeni ya barabara. Wakati kipofu huyu alivyosikia sauti za umati kama ilivyokawaida alitaka kujua nikitu ghani kinaendelea na anaambiwa kuwa ni Yesu Mnazareti anapita katika njia ile, mara moja baada ya kusikia hilo anapaaza sauti yake “Yesu Mwana wa Daudi unirehemu”. Ni aina ya sala tunayoiita sasa “Sala ya Yesu”. Sala tunayopaswa kuisali kila mara; ni sala ambayo tunaweza kuisali kwa uaminifu wakati tunapokubali kwamba sisi tunahitaji msaada wa Yesu na kuongozwa naye, na wakati tunapotambua nakukubali kwamba tupo mbali sana na kile alichotuitia Yesu tukiishi.
Maelezo ya yule kipofu ni maneno ambayo yanamfaa kila mmoja wetu anayemtambua Yesu. Sisi bila Yesu, ni vipofu, hatuwezi kuona vizuri ingawaje tunaweza kujiona wenye akili na maarifa mengi, tuliyosoma sana. Sisi ni waombaji. Tunaweza kumfuata Yesu kweli kama tutatambua kwamba, hata tuwe na akili ya namna ghani, maadili ya namna ghana au mali nyingi kiasi ghani, sisi kwa hakika ni masikini. Yule kipofu alikuwa amekaa kando ya barabara, sio barabarani. Na hii ndio maana halisi ya anaye kaa kando ya barabara, kwamba ni mwombani na kipofu kweli. Barabara au njia kwenye habari iliopo kwenye Injili ni ishara inayoonesha kwamba Kristo ni njia. Aliye na ukweli na uzima wote. Kwahiyo mwishoni mwa ujumbe wa Injili, baada ya yule kipofu kukutana na Yesu sasa anaweza kuona tena, yeye sio muombaji tena, na anafuatana na Yesu barabarani, njiani. Nasi tuliokutana na Yesu katika ubatizo, tutembee katika njia yake.
Sala: Yesu Mpendwa, naomba niweze kuona vyema katika wewe. Amina.
Copyright ©2013-2026 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment