Kiitikio. Zaburi: Zab 25:4-5, 8-10, 14, Mungu ni rafiki kwa wale wote waliokaribu naye.
Somo la 2: 2 Thes 3:12-4:2, Paulo anawambia Wathesalonike kwamba kitu kizuri cha kufanya wakati wanamngojea Masiha ni kupendana kati yao.
Injili: Mk 21:25-28.34-36, Luka anawaonesha Jinsi Yesu anavyo ongelea kuhusu nyakati za Mwisho na hivyo anawaalika watu wawe macho, kwani hawajui siku wala saa atakapokuja.
_______________________________________________________
MAJILIO: KUWA TAYARI, KUWA MAKINI
Kanisa lina nyakati mbali mbali. Vipindi mbali mbali kukumbuka ukombozi wa Mungu, upendo wakujitoa. Katika kipindi hiki kanisa linatufundisha katika hali ya undani, kutoa nyakati za kuongeza imani, ili tukiwa tumejiandaa tunampa Bwana nafasi ya kujitoa kwetu katika hali ya ukamilifu kwetu.
Majilio ni Kipindi maalumu cha kujiandaa kwa ajili ya sherehe ya Noeli. Majilio maana yake ujio au "kuja", maandalizi ya ujio wa Mfalme. Kiliturjia, ni maadhimisho ya kipindi kilichopita, historia ya kuzaliwa Yesu. Kuzaliwa kwa Yesu kama Mwanadamu tayari imeshatokea. Maandalizi yetu hayapo kama yale ya Waisraeli wanaosubiri wakati ujao. Lakini kama Israeli mpya, tunaishi wakati ujao kwa uhakika wa kuzaliwa Bwana, na pia kwa ujio wake wa sasa. Maisha yetu yote ni Majilio, wakati ambao Bwana atakuja. Ingawaje ameshakuja kwa kila mmoja wetu, hajaja katika ukamilifu wote. Tunajilinganisha na wale wa zamani waliokuwa wanamsubiri Bwana. Kwa kuingia katika hali yao, tukijenga matamanio yetu kama ya kwao, matumaini yao, tunasukumwa kutamani ujio wao zaidi na zaidi, tunajitakasa na kujiandaa kwa ujio wake.
Tukiwa tunajiandaa katika hali ya Sakramenti, Bwana anakuja, Kanisa linatangaza, andaa moyo wako kwa ujio wake, hatufanyi kama maigizo bali tunafanya kwa moyo kabisa ndani ya Liturjia. Bwana anakuja katika hali ambayo hajawahi kuja kabla. Tunaingia katika mafumbo ya majilio tukiwa na imani thabiti, tukiwa na shauku, kutamani, tukiamini kwamba Mungu anajitoa kwetu katika hali ambayo hajajitoa tena kabla. Atakuja, tunatazamia tukiwa na mapendo makuu.
Jaribu kufikiri kwa mfano unashanga unamkaa asubuhi na leo ni Noeli alafu umesahau kuandaa! Huna chakula, hujaandaa nguo, wala hujapamba kitu, na huna mpango unaoeleweka. Bilashaka hatuwezi kuruhusu ali hiyo itokee. Mara nyingi hatujiandai kusherekea vizuri kuzaliwa kwa Yesu katika mioyo yetu. Kipindi cha Majilio ni kipindi cha kujiandaa kumkaribisha tena Yesu ndani ya mioyo yetu.
Ni kwa kuwa na moyo wa unyenyekevu ulio makini. Mchezaji mzuri wa mpira ni yule aliyeweka mawazo yake katika ule mpira na wachezaji wenzake. Mwanafunzi mzuri ni yule anayeweka mawazo yake darasani na kusikiliza anacho fundisha mwalimu. Mkatoliki mzuri ni yule aliyeweka mawazo yake ya roho na mwili kumwelekea Mungu, akijiingiza kwenye sala daima na kufanya matendo ya huruma. Tunatambua kuwa Noeli itakuja tarehe 25, mwezi wa 12. Tutakuwa tunaimba nyimbo mbali mbali, kanisa na mazingira yetu yatapambwa vizuri na nyota na maua mbali mbali, watu watanunua nguo mpya. Yote haya ni mazuri. Lakini uwepo wa Kristo tusiuchukulie katika hali hii tu. Yeye anakuja katika hali ya ukimya wa roho zetu ili tuweze kukuwa naye katika mioyo yetu! Tunapaswa kujiandaa kwa kuungama dhambi zetu vizuri na kutakasa roho zetu. Lakini pia lazima kutambua kuungama tu ya zamani sio alama ya kukuwa na kuwa na hali njema. Tunapaswa kukuwa katika upendo na Mungu. Kama vile kuzaliwa kwa Yesu, Mungu alikuwa karibu kabisa na ubinadamu, tunapaswa kukuwa katika utakatifu na tunapaswa kukutana na Yesu. Kukuwa katika utakatifu maana yake kujifunza jinsi ya kuboresha uhusiano wetu na Mungu kwa sala alisema Mt. Yohane Paulo II.
Tunapaswa kuwa waangalifu na pia kuwa washiriki katika maisha ya sakramenti katika Kanisa. Tunapaswa tuadhimishe Ekaristi katika hali inayofaa, kwani “Kila wakati Kanisa linavyo adhimisha Ekaristi linakumbuka ahadi yake na kujikita katika yeye “ambaye atakuja”. Katika sala zake linaita ujio wake. “Maranatha!” “njoo Bwana Yesu” Bwana tunaomba neema zako zije na ulimwengu utapita. (Katakisimu ya Kanisa katoliki – 1403)
Tamaa ya kutaka kuwa karibu na Yesu inapaswa kuwa ni tamaa pia ya kutaka kuwa karibu na ndugu zetu, dada na kaka zetu, kwani hakuna kitu kizuri kwa Mungu kama kutamani ishara ya huruma ya kweli. Kwa hali yake ya asili huruma na inakuwa inaonekana katika hali ya matendo Fulani. Hatuitwii tu kuwa karibu na Mungu bali pia tunaitwa kwakuwa karibu huko kuleta mabadiliko katika maisha yetu na kwa wote walio karibu nasi,hasa maskini, wagonjwa na wanaoteseka. Tunaomba neema ya majilio itusaidie kuwa wanyekevu ndani ya mioyo yetu.
Sala: Bwana, majilio inavyoa anza, mioyo yetu inatamani kupata joto la upendo wako na akili zetu zinatafuta mwanga wa Neno lako.Tuongezee Imani Mkombozi wetu ujasiri na kukuwa katika upendo. Nisaidie niweze kufungua masikio yangu na kusikia sauti yako, na moyo wangu kwa utukufu wako mkuu. Yesu nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment