Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA JANUARI 6, 2024

 

MASOMO YA MISA JANUARI 6, 2024
JUMAMOSI KABLA YA EPIFANIA


SOMO 1
1 Yn 5:5-6,8-13

Wapenzi, Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. 

Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI
Zab 147:12-15, 19-20

(K) Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.

Msifu Bwana, Ee Yerusalemu; 
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni. 
Maana ameyakaza mapingo ya malango yako, 
Amewabariki wanao ndani yako. 

Ndiye afanyaye amani mipakani mwako, 
Akushibishaye kwa unono wa ngano. 
Huipeleka amri yake juu ya nchi, 
Neno lake lapiga mbio sana.

Humhubiri Yakobo neno lake, 
Na Israeli amri zake na hukumu zake. 
Hakulitendea taifa lo lote mambo kama hayo, 
Wala hukumu zake hawakuzijua. Haleluya.

SHANGILIO

Aleluya, aleluya,
Siku takatifu imetung’aria: Enyi mataifa njoni mkambwabudu Bwana: Kwa sababu mwanga mkubwa umeshuka duniani.
Aleluya.


INJILI
 Lk 3:23-38

Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli, wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu, wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai, wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, wa Yuda. Wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri, kwa Melki wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri, wa Yushua, wa Eliezeri, wa Yorimu wa Mathati, wa Lawi, wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu, wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, wa Daudi, wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nashoni, wa Aminadabu, wa Aramu, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda, wa Yakobo, wa Isaka, wa Ibrahimu, wa Tera, wa Nahori, wa Serugi wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala, wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki, wa Methusela, wa Henoko, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani, wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu wa Mungu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Copyright © 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment