JUMANNE, JUMA LA 12 LA MWAKA
SOMO 1
2 Fal. 19 : 9-11,
14-21, 31-36
Senakeribu alituma
wajumbe kwa Hezekia mara ya pili, kusema, Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda,
maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema,
Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru. Tazama, umesikia ni
mambo gani wafalme wa Ashuru waliyozitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa;
je! utaokoka wewe?
Basi Hezekia
akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda,
akaingia katika nyumba ya Bwana, akaukunjua mbele za Bwana. Naye Hezekia
akaomba mbele za Bwana, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya
makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe
ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi. Tega sikio lako, Ee Bwana, usikie; fumbua
macho yako, Ee Bwana, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, ambayo amemtuma mtu
aje nayo ili kumtukana Mungu aliye hai.
Ni kweli, Bwana,
wafalme wa Ashuru wamewaharibu mataifa na nchi zao, na kuitupa miungu yao motoni;
kwa maana haikuwa miungu, bali ni kazi ya mikono ya wanadamu; ilikuwa miti na
mawe tu, ndiyo sababu wakaiharibu. Basi sasa, Ee Bwana, Mungu wetu, utuokoe na
mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe
ndiwe Bwana Mungu, wewe peke yako.
Ndiyo Isaya. mwana wa
Amozi, akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akisema, “Bwana, Mungu wa Israeli, asema
hivi, Kwa kuwa umeniomba juu ya Senake- ribu, mfalme wa Ashuru, mimi
nimekusikia. Tamko alilolitamka Bwana katika habari zake ndilo hili, Bikira,
binti Sayuni, amekudharau, na kukudhihaki sana; binti Yerusalemu ametikisa
kichwa chake juu yako. Maana mabaki yatatoka katika Yerusalemu, na, wao watakaookoka
katika mlima wa Sayuni; wivu wa Bwana utatimiza jambo hilo.
Basi Bwana asema hivi
katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale
hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.Njia ile ile aliyojia, kwa njia iyo hiyo atarudi
zake, wala hataingia ndani ya ya mji huu, asema Bwana. Maana nitaulinda mji
huu, niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.
Ikawa usiku uo huo
malaika wa Bwana alitoka. akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na
themanini na tano elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! hao
walikuwa maiti wote pia. Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akaondoka, akaenda
zake, akarudi akakaa Ninawi.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 48 :1-3,9-10 (K)
8
(K) Mungu ataufanya
imara hata milele.
Bwana ndiye aliye
mkuu,
Na mwenye kusifiwa
sana
Katika mji wa Mungu
wetu,
Katika mlima wake
mtakatifu. (K)
Mlima Sayuni pande za
kaskazini,
Mji wa Mfalme mkuu.
Mungu katika majumba
yake
Amejijulisha kuwa
ngome. (K)
Tumezitafakari
fadhili zako, Ee Mungu,
Katikati ya hekalu
lako,
Ndivyo na sifa yako
hata miisho ya dunia.
Mkono wako wa kuume
umejaa haki. (K)
SHANGILIO
Zab. 130:5
Aleluya, aleluya, Roho
yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelituaminia. Aleluya.
INJILI
Mt. 7:6,12-15
Yesu aliwaambia wanafunzi wake; Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeeni vivyo hivya hiyo” maana hiyo ndiyo torati na manabii. Ingieni kwa kupitia mlango uliyo mwembamba, maana, mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:
Post a Comment