KUFUFUKA
NA KRISTO”
Tafakari
ya Pasaka
Alhamisi,
Aprili 28, 2022
Juma
la 2 la Pasaka
Mdo
5:27-33
Zab
33: 2, 9, 17-20
Yn
3:31-36
KUJAA
NEEMAA: NI KUISHI KATIKA KILE MUNGU ALICHOKUPA!
Wakati
lipo tokea janga linalotokana na asili, au vita vya kisiasa, na chakula ni
vigumu kupata, watu hushikilia na kupangilia kile walicho nacho. Na wasipofanya
hivyo wanaona wanaweza kukosa chakula na kufa kwa njaa. Hivi kama Roho
Mtakatifu ange tuambiae “nitawasaidia kwa kiwango fulani tu. Na kama ukimaliza
neema zako, basi utajitambua mwenyewe” Mmm!
Kwa
neema kwetu, Mungu hutenda tofauti kabisa na sisi. Anatupatia na kutumiminia
Roho Mtakatifu katika hali yote na kutupatia neema zote tunazo hitaji. Shida ni
kwamba hatuzitumii zote, na badala yake tuna acha kuzitumia. Hii si kwamba
hatumwamini Mungu ni mkarimu. Bali ni kwasababu tunaogopa kumruhusu Mungu
amimine nguvu zake katika maisha yetu.
Tujaribu
kufikiria hivi maisha yangu yatafananaje nitakapo mruhusu Mungu afanye chochote
anachopenda katika maisha yangu. Hivi, maisha yetu ya kila siku yangekuwaje,
mahusiano yetu, maneno yetu na wakati wetu ujao hautakuwa tofauti? Tunatambua
kuwa ni haki kumkumbatia Mungu katika kila kitu. Lakini inapofikia sasa ni
wakati wa kukitenda, tunakuwa na wasi wasi mwingi. Inaweza kuwa ni wasi wasi
wakitu kisicho julikana. Au kunaweza kuwa hatutaki kubadilika. Vyovyote
inavyoweza kuwa Mungu anatupa neema zake zisizo pimika kwa kutumiminia Roho
wake. Ni juu yako kuchagua kuamua kumsikiliza na kumchagua au unajipimia na
kuchagua mambo mengine. Kumchagua Mungu ni jambo kubwa kuliko kitu chohcote
unacho weza kufanya katika maisha yako.
Sala:
Bwana, ninataka wewe ufanye chochote unachopenda katika maisha yangu. Ninataka
niingie kabisa ndani ya neema zako. Nisaidie niweze kusema “ndio” kwako bila
kujali chochote kwa utukufu wa kusema “ndio” uliyo niitia. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Copyright
©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment