MBEGU
ZA UZIMA”
JUMAPILI,
FEBRUARI 20, 2022
DOMINIKA
YA 7 YA MWAKA C WA KANISA
1
Sam 26: 2,7-9,11-13, 22-23;
Zab
103: 1-4, 8,10,12-13;
1
Kor 15: 45-49;
Lk
6: 27-38.
------------------------------------------------
WAPENDE
ADUI ZAKO
Vijana
wawili walikuwa wakitembea majina yao ni Smith na Joan wakakutana na kijana
mwingine, Smith akamsalimia huyu kijana lakini chakushangaza huyu kijana
alijibu kwa hasira sana na ukali mwingi. Smith yeye alimjibu kwa utulivu na kwa
upole. Walipo ondoka Joani alimuuliza Smith kwanini yule kijana alikuwa mkali
namna ile? Akamuuliza huwa daima anakufanyia hivyo? Smith akajibu akasema daima
anaongea vibaya ila mimi namjibu vizuri. Joani akamuuliza sasa wewe unawezaje
kuvumilia na hata hukasiriki wakati yeye anakujibu vibaya tena hali ya hasira?
Smith alijibu hivi “kwasababu sitaki yeye awe kwangu kama rimoti yakunifanya
nitende nisivyopenda”.
Haijalishi
ni nanmna gani watu wanaweza kututenda vibaya, bado tunauwezo wakuwarudishie na
kuwatendea Kikristo.
Katika
somo la kwanza Sauli anamtafuta kijana Daudi anataka kumuua. Daudi anapata
nafasi ambayo angeweza kumuua Sauli lakini hakufanya hivyo kwasababu anafahamu
sio sahihi kuua mtu machoni pa Mungu. Katika somo la pili Paulo analinganisha
Yesu na Adamu. Kwa njia ya Adamu tulipata maisha ulimwenguni. Kwa njia ya Yesu
tunapata maisha ya Mbinguni. Katika somo la Injili Yesu anatuambia badala ya
kuwatendea maadui wetu vibaya tunapaswa kuwatendea kwa huruma na kuwasamehe.
Baba
mmoja alikuwa akiishi na mke wake. Alikuwa na mtoto mmoja wa kiume. Baba
alikuwa na bustani yake ambayo alikuwa akiipenda sana. Bustani hi ilikuwa nyuma
ya nyumba yao. Baba alijitahidi kuwafukuza wanyama wakali waliokuwa wakitoka
msituni na kuja kula katika bustani yake. Mbweha alikuwa mnyama ambaye alikua
akija pale. Yule mtoto, Wazazi walimweleza jinsi gani wanyama wa pari walivyo
wakali na kwamba hapaswi kutengeneza nao urafiki kwani watamdhuru vibaya. Daima
Baba alikasirika kwamba wanyama walikuwa wakija kuharibu bustani yake. Baba
alinunua bunduki na daima alikuwa akiipiga hewani ili kuwafukuza wanyama mbali
mbali akiwepo mbweha. Lakini cha ajabu yule mtoto wao alikuwa akiwapenda
wanyama na alitaka kuanza kutenengeneza urafiki na wanyama hawa. Baba aliamua
kuweka fensi kulinda bustani yake.
Yule
mtoto wake alikuwa akitupa chakula nje ya fensi ili kuwakaribisha wanyama
lakini alikuwa akifanya hivi kwa siri ili baba asijue. Siku moja baba aligundua
na alikasirika sana. Akamkataza yule kijana wake. Lakini yule kijana alibuni
mbinu mpya ya kuwapa chakula bila baba kuona, ilifikia mahali wale mbweha
walikuwa marafiki na kuvutwa karibu kiasi ambacho walifikia hata kuchukua
chakula mkononi mwa yule kijana. Baba alipoona alimwambia mtoto wake kwakweli
nilikuwa ninakosea. Kumbe ningeweza kufanya kama wewe, badala ya kuwakimbiza
kwa risasi, kumbe ningeweza kufanya kama wewe, wanyama hao wakabaki na amani na
hata wakati mwingine walikuwa wakija na kukaa na yule kijana pembeni, wakatengeneza
urafiki, badala ya kuwa wanyama adui wakawa wanyama rafiki.
Mara
nyingi sisi wakristo tunajisikia vizuri tunapo acha kurudisha kisasi kwa
majirani zetu. Lakini Yesu alituambia tufanye kitu zaidi, ni lazima tuwapende.
Kumbe kazi ya kufanya ni kuwapenda, na sio kuwakwepa tu. Tunaweza kutambua kuwa
hili kwa ubinadamu ni ngumu sana lakini tunaweza kujifunza kwa yule kijana
katika mfano hapo juu. Licha ya tabia za wenzetu na hali yao ya ukali bado
tunaweza kuwapenda na tusikubali waturithishwe chuki au uadui wao.
Kurudisha
visasi hii ni hali ya kuongeza giza kwenye giza. Mara nyingi tunajenga ukuta
kwa watu tusiowapenda tunatumia nguvu nyingi sana badala ya kutumia nguvu
kidogo na kuwapenda. Chuki haiwezi kuondoa chuki badala yake tupendo waweza
kuondoa chuki. Tuige tabia ya Yesu ya kuwapenda maadui na hata kuwaombea kama
alivyofanya pale msalabani hasa pale wanapotutesa katika maisha. Tusiwe na
tamaa ya kurudisha visasi.
.
Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuwasamehe wale wote walinikosea. Niweke huru
nisiwe muhukumu wa watu na nakuomba tabia hii uijaze huruma yako. Ninakuomba
niweze kuiga huruma yako kamili katika maisha yangu. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
Copyright
©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment