MASOMO YA MISA, JANUARI 24, 2026
JUMAMOSI,
JUMA LA 2 LA MWAKA
KUMBUKUMBU YA MT. FRANSISKO WA SALES
SOMO
1
2Sam.
1:1-4, 11-12, 17, 19, 23-27
Ikawa
baada ya kufa kwake Sauli, hapo daudi aliporudi katika kuwaua Waamaleki, naye
Daudi amekaa siku mbili katika Siklagi; hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja
mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani
mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia. Daudi
akamwambia, Umetoka wapi? Akamwambia, Nimeokoka katika kambi ya Israeli. Daudi
akamwambia, Yalikwendaje? Tafadhali uniambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani,
tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe,
wamekufa.
Ndipo
Daudi akashika nguo zake akazirarua; na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja
naye; wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa
ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana, na kwa ajili ya
nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.
Basi
Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya,
Walio
fahari yako, Ee Israeli juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; jinsi mashujaa
walivyoanguka. Sauli na Jonathani walipendwa na kupendeza maishani wala mautini
hawakutengwa; walikuwa wepesi kuliko tai.
Walikuwa
hodari kuliko simba. Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye
aliwavika mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu. Jinsi
mashujaa walivyoanguka katikati ya vita! Ee Yonathani, wewe umeuawa juu ya
mahali pako palipoinuka! Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu,
ulikuwa ukinipendeza sana; upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, unaopita upendo
wa wanawake. Jinsi mashujaa walivyoanguka wakiwa na silaha za vita
zilivyoangamia!
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
80:1-2, 4-6 (K) 3
(K)
Ee Mungu, uangazishe uso wako nasi tutaokoka.
Wewe
uchungaye Israeli, usikie,
Wewe
umwongozaye Yusufu kama kundi.
Wewe
uketiye juu ya Makerubi, utoe nuru.
Mbele
ya Efraimu, na Benyamini, na Manase,
Uziamshe
nguvu zako,
Uje,
utuokoe. (K)
Ee
Bwana, Mungu wa majeshi,
Hata
lini? Utayaghadhibikia maombi ya watu wako?
Umewalisha
mkate wa machozi,
Umewanywesha
machozi kwa kipimo kikuu.
Unatufanya
sababu ya ugomvi kwa jirani zetu,
Na
adui zetu wanacheka wao kwa wao. (K)
SHANGILIO
Mdo.
16:14
Aleluya,
aleluya.
Ufungue
Moyo wetu, ee Bwana, ili tuyatunze maneno ya Mwanao.
Aleluya.
INJILI
Mk.
3:20-21
Yesu
aliingia nyumbani na mkutano wakakusanyika tena, hao wao wenyewe wasiweze hata
kula mkate. Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana
walisema, Amerukwa na akili.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2026, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment