“ASALI ITOKAYO
MWAMBANI”
Jumamosi, Januari 8, 2022,
1 Yoh 5:14-21;
Zab 149: 1-6.9;
Yn 3:22-30.
KUBAKI DAIMA
KWAKULITAZAMA FUMBO LA NOELI
Karibuni sana wapenzi
wa Bwana kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la Bwana katika
somo la injili, Yohane anafurahi pale asikiapo kwamba Yesu ameanza kubatiza.
Anafurahi kwa sababu anajua kwamba huo ndio ubatizo mkuu kuliko ubatizo
uliofanywa na yeye.
Yesu ameleta ubatizo wa
moto na ubatizo wa Roho. Ubatizo wa namna hii unapaswa umfikie kila mmoja,
upate kuleta upatanisho kamili kati ya Mungu na mwanadamu na kufungua mbingu
ambayo ilifungwa kwa kosa la wazazi wetu wa Mwanzo, Adamu na Eva. Yohane
anakuwa tayari kupisha njia ili ubatizo wa namna hii upate kuifikia dunia,
uiletee furaja na furaha na urafiki na Mungu.
Sisi tujifunze toka kwa
Yohane. Tujiangalie sisi wenyewe kama utendaji wetu unafanania na ule wa
Yohane; isije ikawa uwepo wangu mahali fulani unazuia eneo hilo kupata
maendeleo zaidi. Wapo viongozi walioongoza eneo moja kwa muda mrefu, muda wote
wapo tu pale, lazima ifike mahali wajiulize, je, uwepo wangu katika jumuiya hii
au nafasi yangu imeleta mabadiliko au nimezuia watu wa Mungu kufaidi zaidi?
Tuwe tayari kuachia madaraka, tuwaachie wenzetu, wapo walio wazuri
zaidi-tusifikirie kwamba sisi ndio kila kitu, ati tukiondoka, basi hakuna
kitakachofanyika.
Katika kanisa, upo
uhamisho wa watu mbalimbali, hata kama ni wazuri kiasi gani, watahamishwa tu
ili wasije wakangangania eneo moja na kusababisha ubatizo wa moto na wa roho
kutokea. Tuondokane na dhana ya namna hii. Hivyo, leo tujiulize ni wapi inabidi
tufanye kama Yohane-kuna watu ambao tangu nikiwa mdogo bado ni viongozi
kanisani-wanangangania madaraka yale yale, lazima ifike mahali wajiulize, je,
uwepo wao unaleta baraka zaidi au wanazuia ubatizo wa moto usiwapate waamini?
Yohane hakuwa tayari kuzuia ubatizo wa Moto na wa Roho. Nawe usizuie ubatizo
huu.
Katika somo la kwanza,
Yohane anaendelea kutupatia mawaidha mazuri sana kwamba Yesu ndiye uzima wa
milele. Tukikaa ndani yake twaokolewa na dhambi zote, hata dhambi ya mauti
haitapata mamlaka juu yetu. Na pale tutakapoomba kwa mapenzi yake, tutapokea
tuombalo. Sisi tusiache kumwelekea Bwana Yesu. Yeye ndiye uzima wetu. Hivyo,
tuzidi kumwamini na kumkabidhi maisha yetu yote.
Copyright
©2013-20202 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment