MASOMO YA MISA, DESEMBA 13, 2021
JUMATATU, JUMA LA 3 LA MAJILIO
SOMO 1
Hes 24:2-7.15-17
Siku zile Balaamu aliinua macho
yake akawaona Israeli, wamekaa kabila; roho ya Mungu ikamjia. Akatunga mithali
yake akasema, Balaamu macho asema, Yule mtu aliyefumbwa macho asema; asema,
yeyey asikiaye maneno ya Mungu, yeye aonaye maono ya Mwenyezi, akianguka
kifudifudi, amefumbulia macho; mahema yako ni mazuri namna gani, ee Yakobo,
maskani zako, ee Israeli! Mfano wa bonde zimetandwa, mfano wa bustani kando yam
to, mfano wa mishubiri aliyoipanda Bwana, mfano wa mierezi kando ya maji. Maji
yatafurika katika ndoo zake, na mbegu zake zitakuwa katika maji mengi. Na
mfalme wake atadhimishwa kuliko Agagi, na ufalme wake utatukuzwa.
Akatunga mithali yake akasema,
Balaamu mwana wa Beori asema, yule mtu aliyefumbwa macho asema, yeyey asikiaye
maneno ya Mungu, na kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeyey aonaye maono ya
Mwenyezi, akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho, namwona, lakini si sasa;
namtazama, lakini si karibu; nyota itatokea katika Yakobo; na fimbo ya enzi
itainuka katika Israeli.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 25:4 – 6, 7b – 9 (K) 4
(K) Ee Bwana unijulishe njia zako.
Ee Bwana, unijulishe njia zako,
Unifundishe mapito yako,
Uniongoze katika kweli yako,
Na kunifundisha. (K)
Ee Bwana, kumbuka rehema zako na
fadhili zako,
Maana zimekuwako tokea zamani.
Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili
zako,
Ee Bwana kwa ajili ya wema wako.
(K)
Bwana yu mwema, mwenye adili,
Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi
njia.
Wenye upole akawaongoza katika
hukumu,
Wenye upole atawafundisha njia
yake. (K)
SHANGILIO
Zab. 85:7
Aleluya, aleluya,
Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako,
utupe wokovu wako.
Aleluya.
INJILI
Mt. 21:23 – 27
Siku ile Yesu alipokwisha kuingia
hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha,
wakasema, Ni kwa amri gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa amri
hii? Yesu akajibu, akawaambia, Na mimi nitawauliza neno moja; ambalo mkinijibu,
nami nitawaaambia ni kwa amri gani ninatenda haya. Ubatizo wa Yohana ulitoka
wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu?
Wakahojiana wao kwa wao, wakisema,
Tukisema, Ulitoka mbinguni, atatuambia, Mona basi hamkumwamini? Na tukisema,
Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni
nabii. Wakamjibu Yesu wakasema, Hatujui. Naye akawaambia, Wala mimi siwaambii
ninyi ni kwa amri gani ninatenda haya.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment