MASOMO
YA MISA NOVEMBA 4, 2021
ALHAMISI,
JUMA LA 31 LA MWAKA
SOMO
1.
Warumi
14:7-12
Kwa
sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa
nafsi yake.
Kwa
maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi
kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.
Maana
Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai
pia.
Lakini
wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako?
Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
Kwa
kuwa imeandikwa,
Kama
niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu;
Na
kila ulimi utamkiri Mungu.
Basi
ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
Neno
la Bwana.......Sifa kwako ee Kristo.
WIMBO
WA KATIKATI
Zaburi
27:1,4,13-14 (K)13
(K)Naamini
ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai.
BWANA
ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope
nani?
BWANA
ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu
nani?
(K)
Neno
Moja nimelitaka kwa BWANA,
Nalo
ndilo nitakalolitafuta,
Nikae
nyumbani mwa BWANA
Siku
zote za maisha yangu,
Niutazame
uzuri wa BWANA,
Na
kutafakari hekaluni mwake.
(K)
Naamini
ya kuwa nitauona wema wa BWANA
Katika
nchi ya walio hai.
Umngoje
BWANA, uwe hodari,
Upige
moyo konde, naam, umngoje BWANA.
(K)
SHANGILIO.
Mathayo
11:28
Aleluia
Aleluia
Njoni
kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Aleluia!
INJILI.
Luka
15:1-10
Basi
watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize.
Mafarisayo
na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi,
tena hula nao.
Akawaambia
mfano huu, akisema,
Ni
nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini
na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
Naye
akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.
Na
afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia,
Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.
Nawaambia,
Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja
atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya
kutubu.
Au
kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na
kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
Na
akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja
nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
Nawaambia,
Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi
mmoja atubuye.
Neno
la Bwana......Sifa kwako ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment