MASOMO
YA MISA NOVEMBA 22, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 34 LA MWAKA
SOMO
1
Dan.
1:1-6,8-20
Katika
mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehohakimu, mfalme wa Yuda, Nebukadreza, mfalme
wa Babeli, alikwenda Yerusalemu akauhusuru. Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa
Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye
akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile
vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake.
Mfalme
akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matoashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli,
wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; vijana wasio na mawaa, wazuri wa
uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu;
tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Huyo mfalme
akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza
walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya
mfalme.
Basi
katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli,
na Azaria. Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa
chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamomba yule mkuu wa
matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. Basi Mungu alimjalia Danieli kupata
kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi. Mkuu wa matowashi
akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi
chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi
kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa
change mbele ya mfalme.
Ndipo
Danieli akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya
Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria, Tafadhali utujaribu sisi watumishi
wako muda wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe. Kisha nyso zetu
zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme;
ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona. Basi akawasikiliza katika
jambo hilo, akawajaribu siku kumi. Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao
zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana
wote waliokula chakula cha mfalme. Basi yule msimamizai akaiondoa posho yao ya
chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu.
Basi,
kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na
hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto. Hata
mwisho wa siku zile alizoagiza mfalme za kuwaingiza, mkuu wa matowashi
akawaingiza mbele ya mfalme Nebukadreza. Naye mfalme akazungumza nao; na
miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na
Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme. Na katika kila jambo
la hekima na ufahamu aliowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi
ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Dan.
3:52-56 (K)
(K)
Wastahili kusifiwa na kuadhimishwa milele.
Umehimidiwa,
Ee Bwana, Mungu wa baba zetu,
Wastahili
kusifiwa na kuadhimishwa milele.
Limehimidiwa
jina lako takatifu, tukufu;
Lastahili
kusifiwa na kuadhimishwa milele. (K)
Umehimidiwa
katika hekalu la fahari yako takatifu,
Wastahili
kusifiwa na kutukuzwa milele. (K)
Umehimidiwa
utazamaye vilindi,
Uketiye
juu ya makerubi;
Wastahili
kusifiwa na kuadhimishwa milele. (K)
Umehimidiwa
katika anga la mbinguni,
Wastahili
kusifiwa na kutukuzwa milele. (K)
SHANGILIO
2Tim.
1:10
Aleluya,
aleluya,
Mwokozi
wetu Yesu Kristu alibatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa
Injili.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:1-4
Yesu
aliinua macho yake akawaona matajiri wakiitia sadaka zao katika sanduku la
hazina. Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. Akasema, Hakika
nawaambieni, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; maana, hao wote
walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia
vyote alivyokuwa navyo.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment