“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi,
Novemba 6, 2021
Juma
la 31 la Mwaka wa Kanisa
Lk
16:9-15
KIZAZI
CHENYE KUWAJIBIKA.
Kutambulishwa
na kukuwa kwa teknologia imeleta msaada mkubwa sana katika maisha yetu ya kila
siku, lakini kwa upande mwingine ni kama imetukata mikono. Tunaona watu wengi
muda mwingi wakiwa na simu zao, tableti na kompyuta wakiangalia facebook,
meseji za whatsapp, Twitta nk. Tunaona watu wanashugulika zaidi na simu kuliko
watu walionao karibu. Mbaya zaidi wengine wakichati hata wakati ule wakula
kwenye familia, au hata wakiwa wamealikwa kwenye sherehe watu hawaongei tena,
wako bize na sumu zao. Mikono yetu imekatwa na teknologia hatuwezi tena
kusaidia wengine, na wala hatuna tena muda wakuongea kijumuiya. Tumetekwa
kifikra na kiakili hatuweze kuongea na wenzetu walio karibu nasi, tukiulizwa
swali tunasema tuu ndio au hapana na wala hatujui kwanini tumesema hivyo,
kwasababu akili na mawazo yetu hayapo pamoja na wengine walio karibu. Tunaishia
kwenye ubinafsi. Kuhusu hili limewashika wengi na ni vizuri kujichunguza,
tunapoteza ile furaha na upendo wa kuongea na ndugu walio karibu nasi.
Ni
dhahiri kwamba, tuna tabia ya kutupa ya zamani na kutaka mapya. Nguo mpya, simu
mpya, magari mapya nk. Sasa tunataka kutupa tamaduni zetu njema na kuiga
tamaduni zinazo haribu asili yetu kama wanadamu. Tunadharau hata tamaduni zetu
zenye maadili mema tukidhani mambo mapya ndiyo yenye maana.
Masomo
ya leo yanatualika tuwe mawakili waaminifu katika kutumia vitu vyetu
tulivyonavyo. Je, vitu vyetu vinatuweka karibu na Mungu au ndio vinafuta hata
kile kidogo nilichonacho? Tumetumia vipaji, zawadi na mali zetu na wengine? Je
tumekuwa watumwa wa vitu tulivyo navyo? Hatuna wasi wasi kwamba mali tulionayo
ni Baraka kutoka kwa Mungu kama tumeyapata kwa haki na maadili mema. Kwanza
kabisa kama Wakristo, tunapaswa kutumia vyote tulivyo navyo kwa faida ya
wengine. Pili, kama mmoja akiwa mwaminifu katika kushirikisha ya duniani, Mungu
pia atamshirikisha utajiri wa Mbinguni. Na tatu, tutambue utajiri wa duniani
una thamani ya duniani.
Paulo
anakiri kwamba, Wafilipi wamekuwa Kanisa pekee lililokuwa na ukarimu kwa mali
zao wakati akiwa gerezani, akipata mateso. Walimpatia msaada kila mara. Na
zaidi sana, ilikuwa ni sadaka safi yenye kumpendeza Bwana. Je, waliitikia vipi
kuhusu mahitaji ya Paulo akiwa gerezani? Walikusanya mchango kwa upendo na
kumpa Epafra, ampelekee Paulo mahitaji. Na mwisho kabisa walilisaidia kanisa na
kutumia utajiri wao kwa ajili ya wengine.
Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuwa muwajibikaji wa kushirikisha nilivyo navyo
utajiri wa mali na utajiri wa kiroho. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment